ZIJUE SIKU HATARI ZA KUPATA MIMBA.

Image result for mzunguko wa hedhi

N akama hujaelewa nipigie simu kwa 0753121916 ili nikueleweshe.

Muhimu kwanza ni kujua mke wako (au mwanamke wako sijui mkuu) ana mzunguko wa siku ngapi.
Wapo wa siku 28, 35 etc. Kufahamu hasa hesabu kuanzia siku ya kwanza ya hedhi ya mwezi huu hadi siku ya kwanza ya hedhi ya mwezi ujao. Wengine hesabu zao ziko irregular, hapo ni mtihani kidogo.
 Wengine ni regular, yani mathalan, siku 28 kwa kila mwezi. Tutapigia mfano kuwa mtu wako ana mzunguko wa siku 28, siku ya kwanza ya mzunguko ikiwa ni siku ya kwanza kupata hedhi (na SI siku ya kwanza ya mwezi kwenye kalenda. Yani sio tarehe 1 Januari, au 1 Februari, ingawa labda ya mtu wako ikawa inaingiliana na tarehe za kalenda, hilo sifahamu).

 Sasa basi, kufahamu lini ni siku za hatari kwa mtu wako (siku za Ovulation...yani yai kutoka), chukua idadi za siku katika mzunguko wake, ambazo hapa tutaassume kuwa siku 28, toa siku 14 kutoka hapo (28-14=14). Jibu letu ni 14, hivyo siku ya 14 tangu aanze kupata hedhi ndiyo siku atakayo ovulate (yani kutoa yai). Ukikutana naye faragha katika siku hiyo kuna uwezekano mkubwa akabeba mimba.

 Aidha, wakati mwingine huwa mzunguko hauko sawa, hivyo kitaalamu unaongeza siku 2 mbele na unatoa siku 2 mbele, na kwa hivyo ukikutana naye siku ya 12, 13, 14, 15, 16 zote ni siku za hatari. Literature nyingine zinataka uongeze siku 3 mbele na siku 3 nyuma (iwe tarehe 11, 12, 13, 14, 15, 16, na 17). Na sababu nyingine kubwa ya kuongeza siku 2 (au 3) mbele na nyuma ni kuwa sperm (seli ya uzazi ya kiume) inao uwezo wa kukaa kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa siku 3 (masaa 72) ikiwa hai na ovum (seli ya uzazi ya mwanamke) inao uwezo wa kukaa hadi siku 2 (masaa 48) kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke ikiwa hai. Hivyo basi, unaweza kukutana faragha na mtu wako leo, mathalani ni siku ya 12 ya mzunguko wa mwanamke wako, sperms zako zikakaa siku 2 hadi 3 zikiwa hai, zikaja kuchavusha (kufertilize) ovum yake baada ya siku 2 na ukabaki unashangaa kwanini amepata ujauzito. 

Na kama kuongezea tu, mwanamke anapofikia kwenye siku ya kuovulate (kutoa yai) huwa ana mabadiliko fulani ya kifiziolojia yanayompata. Mfano, atakuwa na joto la mwili lililopanda kiasi, atakuwa ana hamu kubwa zaidi ya kukutana faragha na mwanaume n.k, kutokana na mabadiliko ya kihomoni anayoyapata mwilini mwake wakati huo. Natumai nimejibu swali lako ipasavyo mkuuz

Post a Comment

أحدث أقدم