MESEJI ZENYE KUVUTIA ZA MAPENZI.

 


Upendo uso kipimo, wewe nimekupatia, Moyo unalo tuwamo, raha naipata pia, Kwenye moyo wangu umo, raha yangu ya dunia, Siogopi kukupenda, hata watu wakisema.

Wenye kusema waseme, waseme hadi wachoke, Roho zao ziwaume, ziwaume wakereke,Mioyoni ziwachome, wachomeke wakauke, Siogopi kukupenda, hata watu wakisema.

Wenye wivu uwashike, uwashike uwagande, Zaidi wahuzunike, wahuzunike wakonde, Chakula kisiwashuke, wacha mie nikupende, Siogopi kukupenda, hata watu wakisema.


Post a Comment

Previous Post Next Post