SMS ZA KUOMBA RADHI KWA MPENZI PART 1

Hivi kweli haya ndiyo mapenzi ama naota njozi? Nimefanya kila naloweza kuliimarisha letu penzi lakini naishia kuambulia majonzi, nimekuwa mtu wa kububujikwa na machozi kwa sababu ya lako penzi, kama nimekukosea tafadhali niwie radhi mpenzi, nakupenda na amini wewe pekee ndiye uliyetimiza ndoto yangu ya mapenzi. 
______________________________________ 

Hivi ni kosa gani nilililokutendea ambalo sipaswi kusamehewa? Ni kweli nilikosea nahitaji kusamehewa mpenzi, plz naomba nielewe kwani sina mwingine zaidi yako wewe. Luv u 
_______________________________________ 


Nakiri kweli nimekukosea naomba wako msamaha kwa yote yaliyotokea hakika nimekukwaza 
lakini kwa hakika hii ni mara yangu ya kwanza naamini,naamini utanisamehe laaziz 
na kunipa nafasi ya kulienzi lako penzi. 
_______________________________________ 


unajua nakupenda ila tu umeamua kunitenda rudisha moyo nyuma kasha twende sambamba mapenzi yanavyokwenda. 
_______________________________________ 

Mapenzi ni usaníi ukiigiza utashindwa,mapenzi yanatoka moyoni wengi walioigiza walishatengana,mpenzi wangu usiniache. 
______________________________________ 
penzi la kweli siku zote hudumu,penzi la kitapeli haliishi ugomvi,mpenzi wangu leo nimegundua nakukosea na naahidi kubadilika na kuwa mpenzi mpya na bora,nisamehe . . 
_______________________________________ 

mpenzi nashukuru nikikuacha nitakuwa ninakufuru mi ndiyo mpenzio na hauna mwenzako mpenzi kuwa huru. 
_______________________________________ 


Japo umeniuzi sina budi kukupa hizi pongezi, sijui umejifunza wapi mapenzi, hakika kwako mi ni mfungwa wa mapenzi! Nakupenza mpenzi nitunziye langu penzi! 
_______________________________________ 

Hakika sikutaraji kulikosa lako penzi, wataka kuniacha kuniacha ningali nakuhitaji, mpenzi tambua nahitaji yako hifadhi na niko radhi kukupeleka hadi kwa wangu wazazi, amini kwenda kwa mwingine sihitaji. Nakupenda. 
_______________________________________ 

Siamini kilichotokea, hakika nimekukosea, lakini naapa katu sitorudia, upuuzi niliokufanyia, najua jinsi gani waumia ndiyo maana umeninunia, nisamehe mpenzi nafsi yangu ipate kutulia kwani bila wewe sin thamani katika hii dunia! 
_______________________________________ 

Kina ninapokukumbuka machozi yanidondoka, hivi leo mwana wa mwenzio ninaumbuka kwa kuparamia mapenzi kwa pupa, ukweli nakupa, hivi sasa najuta! Nisamehe mpenzi. 
_______________________________________ 

Ni kweli nakiri ndani ya nafsi yangu kwamba nilikukosea mpenzi wangu, naomba unisamehe na unipe nafasi nyingine katika moyo wako mpenzi wangu. Nakupenda sana, pokea busu mwanana....mwaaaaaaaa. 

Post a Comment

أحدث أقدم