KUNA HATUA KABLA YA KUZAMA PENZINI USIKOSEE!

 


 raha yake ni kupendana. Yananoga zaidi wapendanao wanapopendana kwa asilimia mia. Mwanaume ampende mwanamke kwa kiasi hicho, vivyo hivyo mwanamke ampende mwanaume.  

Hapo ndipo utaiona tamu ya penzi. Wataalamu wa masuala ya uhusiano wanakuambia pendo la kweli halifi (true love never die).

Halifi kwa sababu linatoka moyoni. Anampomweka mwenzake moyoni, hapo anakuwa tayari kwa lolote. Ni kama vile imani, inamshika kwelikweli.

Humwambii kitu.Kweli kuna raha yake mtu kama huyo kumpenda mwenzake kiasi hicho. Inapendeza zaidi pale tu anayependwa, naye akarejesha upendo huo. Tofauti na hapo, penzi linageuka mateso.

Mmoja anampenda mwenzake, mwenzake hampendi. Kwenye jamii zetu haya tunayaona, wapo wanaume ambao wanawapenda sana wapenzi wao, wanawake nao wanarejesha upendo. Wanathaminiana, wanajaliana kiasi cha kuzua gumzo haswa kwa wale ambao wanakosa penzi la kweli.Mtu anampenda mpenzi wake mpaka anaumwa.

Anatamani kuwa naye kila wakati, anamuonesha kila linalopaswa kufanyika kudhirisha upendo. Hapo ndio utasikia yale maneno ya ‘fulani na mpenzi wake wanapendana hadi raha’.

Upendo unapofikia hatua hiyo, ndiyo pale zinapozaliwa kauli za ‘mimi siwezi kuishi bila ya yeye.’ Au kauli kama ‘maisha yangu si chochote bila yeye.’ Anamweka mpenzi wake katika fungu la kwamba likitokea la kutokea, ataumia sana.Yaani kwa jinsi alivyompenda, siku akiambiwa tuachane anachanganyikiwa.

Hataamini kilichotokea. Anateseka kwa mwezi mmoja, miwili hata mwaka. Anaumia kwa sababu alimpenda kwa dhati mpenzi wake. Alimuweka moyoni. Hapo ndipo kwenye kiini cha mada yangu, kama nilivyotangulia kusema katika kichwa cha habari, mpende mtu sana lakini ni muhimu kujifunza kuweka akiba.

Kabla ya kufikia hatua ya kumuweka mtu moyoni, hakikisha kwamba unayetaka kumweka ni mtu sahihi.

UTAMJUAJE MTU SAHIHI?

Mara kadhaa nimekuwa nikisema, mtu sahihi utamjua kwa matendo yake. Unapokuwa kwenye hatua za awali za uhusiano, ni rahisi sana mtu kuficha ‘madhambi’ yake lakini hawezi kuficha kwa wakati wote. Atakuficha kwa miezi miwili mitatu lakini ndani ya mwaka mmoja au miwili utamjua tu.

CHEKECHA AKILI YAKO

Ruhusu akili yako ipambanue mambo yanayohusisha penzi lenu. Waza kwa kina kila hatua mnayopitia. Usimweke mtu moyoni kabla hujajiridisha kama ana mapenzi ya dhati. Ana malengo na wewe? Hatamani tu kitu fulani kutoka kwako?

WEKA AKIBA

Katika kipindi cha awali, jifunze kuweka akiba. Muoneshe upendo, mjali na umthamini lakini katika akili yako weka akiba ndogo kwamba siku akisema hanitaki itakuwaje? Akisema kila mtu achukue njia yake itakuwaje? Akiondoka duniani je? Hutapagawa? Rafiki yangu, nakushauri. Kwa ustawi wa uhai wako ni vyema ukawa na akiba japo kiasi katika pezi lako. Hiyo ni kama tahadhari ambayo itakusaidia pindi litakapotokea la kutokea. Usiumie. Usichanganyikiwe na kujikuta ukipata matatizo yanayoweza kukuondoa duniani.

MAPENZI YANAUA

Ni kweli kabisa, tumeshuhudia matukio mengi ya watu kuuana kwa sababu ya usaliti, kwa sababu ya wivu na mambo mengine kama hayo. Maafa kama hayo yasingetokea kama wahusika wangekuwa wameweka akiba ya upendo.

PENDA TARATIBU

Usiingie mzima mzima katika mapenzi. Ingia kwa tahadhari. Hakikisha unacheza vizuri katika uhusiano wako, jitambue na usikubali kuchanganyikiwa sababu ya mapenzi. Upendo wa kweli unaishi. Mtaishi kwa muda mrefu mkisomana, mkishibana na mwishoni mtafikia kwenye hatua ya upendo wa kufa na kuzikana.

Post a Comment

أحدث أقدم