Sheria Za Kufuata Unapomtumia Meseji Uliyemzimia.

Umepewa nambari ya simu na mwanaume/mwanamke unayemzimia na hujui aina gani au ngapi za meseji unazotaka kumtumia? Cheza kwa ujanja ukitumia sheria hizi ambazo ni lazima yeyote anafaa kutumia ikija maswala ya kumtext yeyote aliyemzimia.




1. Mtext unayemzimia kwa maswali rahisi
Kama unamtaka yule uliyemzimia ajibu texts zako, lazima utoe sababu muhimu kwake kujibu texts zako. Unaweza kuanza kumtext kwa kumuuliza anafanya nini muda huo ama unaweza kumtext na kitu ambacho mlikuwa mkifanya pamoja wakati uliopita. Mfano unaweza kumtext 'Ile story ya kuenda kumtembelea binamu yako ilifikia wapi?'

2. Usingojee ajibu meseji ukiwa hapo
Iwapo amejibu text yako kwa haraka ni vyema. Lakini kama atachukua muda mwingi, usijisumbue kamwe kukaa karibu na simu. Tafuta kazi nyingine ile ujikeep buzy usijishughulishe na kufikiria meseji uliyomtumia.

3. Usimtext unayemzimia meseji nyingi wakati mmoja
Usijaribu kutuma zaidi ya meseji moja kabla hajakujibu. Hii itaondoa ile hisia ya kuonekana kama mtu mwenye tamaa ama kuonekana kama una ajenda chafu. Hii itajitokeza iwapo kama huyo unayemzimia hujakuwa na mazoea naye.

4. Mazungumzo yenu yaendelee...hadi pale kikomo
Iwapo maongezi yenu yanaendelea vizuri basi ni vyema. Hakikisha ya kuwa usipitishe maongezi yenu mpaka yaingie kitengo cha kuboesha. Ukiona unayemzimia anachukua muda mrefu kujibu texts zako ama kujibu kwa neno moja moja, basi fahamu ya kuwa maongezi yenu yamefika kituo na unafaa kusmamisha texts zenu hadi siku nyingine.

5. Endeleza maongezi binafsi
Kutumia mtu meseji ni rahisi sana kwa kuwa inatoa tenshen na wasiwasi. Pia meseji husaidia mtu kujieleza zaidi. Lakini unafaa kufahamu ya kuwa meseji pekee haziwezi kumshawishi mtu kwa kiwango kikubwa hivyo unafaa ufuatilie wewe binafsi ukutane na unayemzimia ili uendeleze maongezi yenu.
6. Tafuta ishara kubwa kama unayemzimia hajakupenda
Je wewe ni yule ambaye wakati wote unaanza kumtext huyo uliyemzimia?  Je unayemzimia ni yule ambaye anakutumia text wakati wa shida na hawezi kukutext wakati mwingine?  Hii ni dalili ya kuonyesha ya kuwa yule unayemtext kwa kawaida anafanya hivyo ili kuondoa uchoshi kwake ama anafanya hivyo kukuonyesha tu heshima kwako.
Ukiona mtu anamiliki aina hii ya tabia basi ni ishara ya kukuambia ujipatie shughli na utafute kwingine.

Post a Comment

أحدث أقدم