SMS MPYA ZA MAPENZI

 

 Sms 2: Salamu yako ni nusu ya uhai wangu, kuikosa nisawa na kuidhulumu nafsi yangu, kuipata nisawa na ua ridi machoni mwangu, nakila ninapoipata huwa najisikia faraja moyoni mwangu, Nakupenda sana Muhibu wangu.

 Sms 3: Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako, naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA

 Sms 4: Fungua macho yako uone kopa za mahaba ninazokumwagia, fungua mikono yako na upokee mapenzi yangu, fungua simu yako uone ni jinsi gani ninavyokukumbuka japo kwa kukutumia sms mpenzi wangu, Nakutakia usiku mwema

 Sms 5: Utamu wako ni zaidi ya asali, ni wa asili usiohitaji kuongezewa ladha ya sukari, nitaumiss endapo kama ukiwa mbali "NIACHE NIKUPENDE SWEET"

Sms 6: Moyo wangu umehifadhi hisia zako, nakuahidi kamwe sintopunguza upendo kwako, tunza sms hii ya ahadi kwenye simu yako, iwe kumbukumbu kila uisomapo! "NAKUPENDA MALAIKA WANGU"

 Sms 7: Si vibaya mimi kukusifia kwani wewe ni wangu, nivingi umejaaliwa, vinavyouvutia moyo wangu, ama hakika uzuri wako umedhibiti matamanio yangu "SINTOMPENDA MWINGINE ZAIDI YAKO"

 Sms 8: Thamani ya Mapenzi yako nikubwa kwangu, haifanani nachochote kwenye huu ulimwengu, sina budi kumshukuru mungu, kwa kunijaalia mpenzi mwema unaejali hisia zangu, USICHOKE KUNIPENDA MPENZI

Post a Comment

أحدث أقدم