Ni lazima uipe pumzi penzi lenu kama mnafanya kazi ambayo inawafanya wewe na mke wako kuwa pamoja kila wakati, basi kila mmoja anahitaji muda wa peke yake awe na muda wa kummiss mwenzake.
Huwezi kummiss mtu ambaye kila dakika unamuona, sana sana utaishia kuona mapungufu yake na kugombana tu. Utammiss vipi wakati kila wakati uko naye, kila mmoja anahitaji kummiss mwenza wake ili mapenzi yawe na raha.
Mume/mke wako anahitaji maisha mbali na wewe, anahitaji angalau nusu saa kwa siku ambayo hataona sura yako, atakuwa na watu wengine, atakuwa na marafiki au atakuwa anafanya kitu kingine bila wewe.
Kama uko kwenye ndoa au mahusiano ambayo kila kitu mnafanya pamoja, kila wakati mko pamoja, kila muda wa ziada mko pamoja basi suala la kugombana kwenu ni la muda tu.
Jifunze kuwa na furaha nje ya mwenza wako, si kuchepuka hapana, hata kucheza tu karata na majirani inatosha kukufanya ummiss mwenza wako.
Kama kila wakati mko pamoja, hata kama hamfanyi kazi pamoja lakini kama ule muda wa zaida kila siku mpo pamoja basi mtaanza kuboana, utaanza kuona mapungufu ya mwenza wako, utaanza kuona ubaya wake na mtagombana tu.
Yes kuna watu wanalalamika kuwa waume zao wanawaganda hawatoki nyumbani, kuna wanaume hulalamika wake zao wanawaganda.
Kama mnagandana kama mapacha halisi jua tu mtaboana.
Post a Comment