Jinsi ya kuyanogesha mahusiano yenu ya kimapenzi.

 

Leo ninakupa njia nne zitakazolifanya penzi lako liendelee kunoga, hata kama litakuwa limeanza kufubaa utaliamsha upya.
Wengi wamekuwa hawaelewi mambo mengi kuhusu uhusiano ndiyo maana huishia kulalamika kwamba wanapenda sana lakini mwisho wa siku huishia kutendwa.
Hakuna mtu ambaye hahitaji faraja, kila aliyekuwa na mpenzi wake anahitaji kuwa na furaha. Hakuna mtu ambaye anaingia kwenye mapenzi ili apate msongo wa mawazo, kila mtu anayediriki kuutoa moyo wake, kitu cha kwanza anachokitarajia ni faraja kisha furaha.
Ipo hivyo! Watu wengi wanakuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi huku wakiwa na matumaini kwamba hao waliokuwanao inawezekana watakuwa wapenzi wa maisha yao yote. Pasipo kujua, wakati mwingine kuna makosa hufanyika, mtu hajui afanye nini ili penzi alilonalo kwa mpenzi wake linoge, hajui ni njia zipi zitamfanya kupendwa kila siku.
Leo nitakutajia njia chache ambazo kama utazifanya, nakuhakikishia penzi lenu litashamiri zaidi ya lilivyo hivi sasa.
1. Mpe Uhuru mwenza wako.
Kila mtu anapenda kuwa huru, kuachwa afanye mambo yake anayoyapenda. Hakuna mtu anayependa kuingiliwa, hasa kwenye masuala ya kutumia simu yake. Kama kweli unahitaji penzi linoge, usitake kuingilia mambo yake hasa katika matumizi ya simu, unachotakiwa ni kumwambia muda ambao hupendi kuona akizungumza na simu na si kwamba kila unapoona simu yake inaita, unaichukua kwa nguvu.
Mapenzi hayapo hivyo, mpe uhuru mwenza wako. Haimaanishi mtu kama hajatulia basi kuchukua simu muda wote inapoita ndiyo kutamfanya kutulia, hapana, bali kwa kufanya hivyo utampa mbinu nyingine ya kuweza kupambana nawe. Unachotakiwa ni kumfanya kuwa huru, usimuingilie.
2. Pata muda wa kumtoa out.
Wengi hukosea hapa, huwa hawapendi kwenda matembezi na wapenzi wao. Wengine hujifanya wapo bize, hata ukimwambia Jumamosi nataka tutoke out atakwambia anataka kufanya hili na lile.
Rafiki yangu, kila mtu anahitaji kuwa karibu na mpenzi wake, hakuna anayependa kuwa na mpenzi ambaye muda wote yupo bize tu. Mchukue, nenda naye sehemu. Kutoka mitoko ya mara kwa mara itawafanya muwe karibu zaidi, itawafanya muda wote mzidi kupendana, ila kama utajifanya upo bize, jua kuna mtu ataitumia nafasi hiyo kutoka na umpendaye.
3. Penda kumfanyia utani.
Hakuna mtu anayempenda mpenzi ambaye yupo siriazi saa ishirini na nne. Pata muda wa kukaa na kutaniana naye. Mchombeze kwa vineno vya utani, mpetipeti, mlaze kitandani na uanze kupiganapigana naye vibao vya kimahaba hata kwa kutumia mito ya kulalia.
Unapokuwa siriazi kila wakati inakuwa ni vigumu mwenzako kulifaidi penzi, pendelea kutabasamu inapobidi kila unapokuwa na mpenzi wako, siyo kila atakachokwambia wewe uso wako umekunja ndita kiasi kwamba ataonekana kukuogopa na kumtafuta mtu mwingine ambaye atahitaji kuliona tabasamu lake, atahitaji kuona akifanyiwa utani wa mahaba nk.
4. Penda kumsfia mwenza wako.
Wengi wanaogopa kuwasifia wapenzi wao, hawajui kama kila mtu duniani anapenda kusifiwa. Mpenzi wako anapovaa nguo nzuri zilizomtoa, usikae kimya, mwambie amependeza kwani hilo litamfanya kufurahi sana. Kama utakuwa na mpenzi halafu kila siku humsifii hata akifanya kitu gani, jua kwamba atajisikia vibaya, wakati mwingine atahisi hayupo sawa kwa kuwa tu hujawahi kumsifia.
Unapomsifia mpenzi wako kunamfanya kuongeza umakini katika kuvaa kwake, kununua manukato na hata jinsi atakavyosuka au kunyoa atafanya kwa ubora wa hali ya juu kwa kuwa anajua utamsifia.

Post a Comment

Previous Post Next Post