Ushawahi kugundua ya kuwa wanawake kikawaida huvutiwa na wanaume ambao wana hadhi ya juu? Kama ni kweli, najua kwa akili yako unafikiria ya kuwa iwapo unataka kuwavutia wanawake warembo lazima uwe na umaarufu ama tajiri ama zote mbili. Ni kweli?
Mwanzo kuwa na hadhi ya juu ni nini? Je, kuwa mtu wa hadhi ya juu ina maanisha kuwa tajiri ama maarufu? Ok hebu fikiria hivi: Kama mtu tajiri zaidi ulimwenguni ameamua kusafiri hadi kisiwa flani kisichojulikana ambacho hakina runinga wala redio... mtu huyu atakuwa na umaarufu kiasi gani? Pesa ambazo anazimiliki zitakuwa na umuhimu gani?
Ni hivi, kuwa na hadhi ya juu ni mauzauza. Ni mauzauza ambayo yanajengwa na maoni ya watu ambao unahusiana nao karibu. Mfano, unaweza kuwa na hadhi ya juu ya maingiliano wakati ambapo unatangamana na familia yako, tofauti na kuwa katika chumba ambacho kimejaa watu ambao huwafahamu.
Hivyo kama unataka kuonyesha hadhi ya juu kwa mtu flani, kuna mbinu mbili ambazo unaweza kutumia...
Kwanza: Nufaika na koti ya nyumbani
Katika michezo, kunufaika na koti ya nyumbani inamaanisha kuwa una nambari kubwa ya mashabiki ambao watakupa sapoti na ambao wanayaelewa mazingira uliyomo. Hivyo unaweza kutumia mbinu hii katika maisha yako ya kujamiiana na watu kwa kuchagua sehemu mahususi ambazo utakuwa 'mtu wa kawaida' katika hizo sehemu.
Kwa mfano, kuwa mtu wa kawaida katika baa ama klabu ina maana kwamba unaenda sehemu hizo mara kwa mara, na pia wafanya kazi wote katika sehemu hizo wamekuzoea mpaka wanakujua kwa jina. Kwa ufupi ni kuwa umepandisha hadhi yako ya kujamiiana na wengine katika sehemu hizo kwa sababu unaonekana sehemu hizo mara kwa mara.
Fikiria hili jambo wakati mwingine ambapo utahudhuria sehemu nyingine ambayo hujawahi kuitembelea hata mara moja. Ni tofauti gani ambayo utaihisi iwapo umekuwa ukiitembea sehemu hio kwa miaka mitatu iliyopita? Je si ingekuwa rahisi sana kuwaonyesha wanawake waliokuzunguka kuwa wewe ni mtu wa hadhi ya juu?
Bila shaka ingekuwa... mwanzo kama mwanamke mwenyewe si mtu wa kawaida katika hio sehemu! Ungemtembeza sehemu hio na kumtambulisha kwa "marafiki" zako wafanya kazi pamoja na wateja uliowazoea wa kawaida.
NB: Nenda utafute sehemu mbili ama tatu ambazo utakuwa mtu wa kawaida katika sehemu hizo. Hakikisha ya kuwa sehemu hizo ni ambazo zina wanawake wengi ambao wanaweza kustahili kuwachagua.
Pili: Jenga uhusiano mwema na koti ya nyumbani
Pindi ambapo ushatambulisha sehemu zako ambazo zitakuwa "manufaa ya koti-nyumbani", anza kujenga uhusiano mwema na watu ambao wanakuwa hapo wakati mwingi. Sehemu nzuri ya kuanza ni kwa wafanya kazi, kwa kuwa kila wakati huwa hapo na mara nyingi huwa jamili.
Jifunze majina ya watu na angalau ujue jambo moja linalowavutia. Hakikisha ya kuwa unakuwa mkunjufu kwa wafanya kazi na pia kuwapa bahshishi mara moja au nyingine. Pia usisahau kutambulisha majina ya wafanya kazi wengine iwapo utakumbana na wafanya kazi wengine wapya.
Hii itasaidia kugundua ya kuwa wewe ni mtu ambaye unajulikana na wafanya kazi wale wengine, na itasaidia kuonyesha hadhi kuu kwako kwao. Fanya mazoezi ya mara kwa mara na uwe na subira, na uanze pia kutangamana na wateja wa kawaida katika sehemu hizo.
Kwa muda wa wiki kidogo, itakuwa rahisi kwako kumuonyesha mwanamke yeyote ambaye unakutana naye kuwa wewe ni mwanaume wa hadhi ya juu katika sehemu hizo.
Upo!?
Post a Comment