Njia sahihi ya 7 za kuomba msamaha kwa mpenzi wako.

 Umeshawahi kumkosea mtu na ukashindwa namna ya kuomba msamaha kumaliza tofauti hizo ili kuendeleza uhusiano wenu, kwani mara zote maelewano mabovu hupelekea kuvunjika kwa uhusiano huo, msamaha ndio kiungo pekee kinachoweza kurudisha upendo na amani, Japokuwa watu wengi hawafahamu namna sahihi ya kuomba msamaha ili kusamehewa.



Anaweza kuwa rafiki, mpenzi, ndugu, au mtu yeyote ambaye mna mahusiano na ukamkosea kiasi ambacho utahitaji kuomba msamaha, kwa sababu hiyo unahitaji kufahamu namna sahahi ya kusema neno samahani kwa mtu uliyemkosea, hivyo hapa chini nakuwekea namna bora ya kuomba msamaha kwa mtu uliyemkosea.

1.Beba kosa lako na ukubali kuwa umekosea.

Watu wengi imekuwa mtihani kukubali kosa na kuomba msamaha kwa kuwaumiza wale waliowakosea, iwe jambo la kawaida kuweka majivuno yako pembeni na kulivaa kosa na kuomba msamaha wa dhati mapema iwezekanavyo kwani kadri unavyozidi kuchelewa kuomba msamaha ndivyo unavyozidi kupunguza nafasi ya kusamehewa, Msamaha wa kweli ni ule ambao unauomba kwa dhati kwa kujutia lile ulilofanya na sio kuomba msamaha huku unakumbushia mambo yaliyopita au makosa aliyokufanyia yule uliyomkosea.

2. Mpe zawadi uliyemkosea.

Baadhi ya watu hutuma zawadi kwa watu waliowakosea kkuonesha wanawajali na kuwapenda, kama unataka kuomba msamaha kwa msichana wako unatakiwa kumpatia zawadi ambayo italeta maana kwake mara tu apokeapo zawadi hiyo, maua yanaweza kuwa zawadi nzuri kama tu ni mpenzi wa maua, jitahidi sana kutompa zawadi ambayo haipendi, jitahidi kumpa zawadi ambayo itamfanya ajue kweli unampenda unamjali na unamjua, hii inaweza kumgusa kwa namna ambayo itamfanya akusamehe.

3. Matendo huongea zaidi kuliko maneno.

Kwa kingereza wanasema ”Actions speak laouder than words” unapoomba msamaha onyesha kwa vitendo kuwa kweli unaomba msamaha na unahitaji msamaha wake, watu wengi wanapoomba msamaha wanashindwa kuonesha kwa vitendo kuwa wanaomba msamaha jambo ambalo linawakera sana wale wanaoombwa msamaha kwani kuna muda unataka kumsamehe aliyekukosea lakini matendo yake hayaendani na msamaha wake.

5. Kubali lawama

Unapokuwa unaomba msamaha kubali lawama watu wengi hawapendelei kukubali lawama, ila tambua kuwa unapomkosea mtu huyo anakuwa na mambo mengi anayoyafikiria juu yako ambayo yanaweza kuwa ya kweli au sio ya kweli unachotakiwa kufanya ni kukubali kulaumiwa kwani unapokuwa unakataa inamaanisha bado hujakubali kosa lako hivyo ukimkosea mtu jitahidi kukubali lawama zote ili kumpa nafasi uliyemkosea aone namna unavyojutia kutenda kosa hilo.

6. Ukifanikiwa kusamehewa kuwa mtu mzuri na tofauti

Hapa hutakiwi kurudia makosa, watu wengi hapa wanafeli sana unakuta mtu ametenda kosa kubwa tu ambalo lingeweza kuvuruga uhusiano wako na mpendwa wako, lakini kwa mapenzi na imani kubwa ambayo aliyekosewa anakuwa nayo anaaamua kumsamehe akijua kuwa atabadilika na kuwa mtu bora zaidi matokeo yake aliyekosea baada ya kipindi kadhaa hurudia kosa jambo ambalo kiukweli linakatisha tamaa sana na kumfanya mtu ashindwe kusamehe kwa mara nyingine tena kwani dhahiri inaonyesha ndiyo tabia yake.

7. Tumia nukuu na nyimbo za kuomba msamaha

Nyakati nyingine omba msamah kwa kutumia nyimbo na maneno mazuri ya kuomba msamaha, hii inasaidia kurudisha hisia na kuona kuna haja ya kusamehewa na kurudisha uhusiano uliopo tangu mwanzo.

Kuomba msamaha si jambo jepesi ni ngumu, lakini tumia njia hiz pale unapotakiwa kuomba na msamaha na unapohitaji kusamehewa kwa dhati, watu wengi wanawapoteza wapendwa wao kwa kushindwa kutumia njia sahihi za kuomba msamaha.

Endapo utatumia njia hizi na ikashindikana kusamehewa tambua kwamba huenda mtu huyo akawa amechoka na matendo yako, au huenda ikawa ndio muomba msamaha maarufu katika urafiki wenu, tambua kuwa kila kitu kianachosha, hata misamaha ikiwa mingi inachosha na kufanya uone sio tena kuomba msamaha bali ni kucheza.

Hivyo jitahidi sana pale unapoomba msamaha unakuwa unamaanisha kwa kuomba msamaha wa kweli na kuhakikisha hurudii kosa, japokuwa hata katika maandika yanasema samehe saba mara sabini lakini kibinadamu inachosha na kukatisha tamaa.

Post a Comment

Previous Post Next Post