HATUA ZA KUFUATA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI💋💋

 


❤️Leo Daktari wa Mahaba nawaletea darasa mahususi kuhusu mbinu unazoweza kurudiana na mpenzi wako wa zamani ambaye bado unampenda.
💕 Unajua kuna sababu nyingi zinazofanya watu waachane ilihali bado wanapendana. Siku ingine tutazungumzia sababu hizo ila leo ngoja tuende moja kwa moja kwenye mada.
Unajua kurudiana na mpezi wako wa zamani sio ishara kuwa wewe ni limbukeni au hakuna zaidi yake bali siku zote ni vizuri kuheshimu hisia zako.
❤️Kama bado unampenda na unahisi yeye ni furaha yako sasa kwa nini msirudianae? Labda nikwambie kurudiana na mpenzi wako sio kazi ngumu, kazi ngumu ni kuhakikisha kuwa hamuachani tena. Ebu fikiria kama mtu akiweza kukuacha, utawezaje kurudiana nae na kumfanya hasikuache tena? Kuna umuhimu gani wa kurudiana nae kama mtaweza kuachana tena.
❤️Kuna njia za kufuata ili uweze kurudiana na mpenzi wako wa zamani, kwa sababu pindi tu ulipoachana nae uliumia sana, ulipoteza hisia juu yake na kubwa zaidi ulichanganyikiwa. Na kwa kawaida katika kupindi hichi cha mafarakano, kuna nafasi kubwa ya kufanya makosa ambayo yatakufanaya ushindwe kurudiana na mpenzi wako wa zamani. Katika hatua nne za kufuata ili kurudiana na mpenzi wako wa zamani. Hatua ya kwanza inaeleza makosa ambayo ni muhimu kuyaepuka ili uweze kurudiana na mtu ambaye bado unampenda.
HATUA YA 1. EPUKA MAKOSA HAYA.
(a) kumpigia simu au kutuma sms kila mara.
Ni kosa kubwa sana kumtumia meseji au kumpigia simu mpenzi wako pindi tu mnapoachana. Watu wengi wanafikiri kwamba kuendelea kuwasiliana na Ex wako kutamfanya asikusahau na kukusamehe lakini kitaalam njia hiyo sio sahihi. Unajua unapompigipigia simu na kuwasiliana nae hii ina maanisha kuwa hujiamini na bila yeye huwezi kuishi. Kumwonesha kuwa umamwitaji sana na unateseka bila uwepo wake huwezi kuishi kumtamfanya azidi kuwa mbali na wewe. Hapa kwa wale rafiki zangu wanaotumia vilevi lazima wawe makini sana hasa wanapokunywa pombe na kulewa kupita kiasi hii ni kwa sababu mara nyingi wanapolewa hujikuta wakiwapigia simu ex wao na kitendo hicho huwafanya waonekane wapuuzi zaidi. Najua watu wengi watauliza sasa Eliado nisipompigia wala kumtumia meseji ni vipi ntaweza kurudiana nae? Kuna jinsi ya kuwasiliana nae ambapo utamfanya avutiwe na wewe tena. Ntaeleza jinsi ya kuwasiliana nae katika hatua ya 4.
(b) Kamwe usimwombe msamaha.
Kama msamahaa una maana baada ya kuachana au ni suluhisho basi hakuna watu ambao wangeachana duniani. Unajua mtu akikuacha siku zote anajua utamwomba msamaha. Sababu yoyote iliyowafanya muachane haitobadilishwa kwa kitendo chako cha kuomba msamaha. Kitu cha pekee msamaha kitakusaidia ni kuendelea kuonekana dhaifu na mtu usiyejiweza. Na siku zote tambua ya kuwa hakuwa msichana au mvulana anayependa kuendelea kuwa na mtu dhaifu. Watu wengi wanfikiri kwa kitendo cha kumwambia msichana wako au mvulana kuwa huwezi kuishi bila yeye kitasaidia kumrudisha la hasha utazidi kumpoteza kabisa. Najua hatua hii ni ngumu lakini utanielea tu ndugu yangu.
(c) Usikubali kila kitu anachotaka.
Watu wengi wanafikiri kuwa eti ukimkubalia kila kitu anachotaka atarudiana na wewe. Kwamba vitu vyote vyote si kitu, bali kitu cha muhimu ni kurudiana nae kwa gharama yoyote ile, huo ni upuuzi ndugu yangu. Kuwa tayari kwa lolote hakuta kusaidia kurudiana na mpenzi wako zaidi ya kumfanya akuzarau na kukuona dhaifu sana. Narudia tena ndugu msomaji hakuna mtu anayependa kuwa na mahusiano na mvulana au msichana dhaifu.
(d) Usiendelee kuonesha kuwa unamjali
Najua wengi wanafikiri kuwa eti ukionesha jinsi gani bado unampenda na kumjali mtarudiana. Pia wengine wanajisumbua kumwonesha mtu aliyeachana naye kuwa hakuna mtu mwingine duniani anaweza kumpenda jinsi anavyompenda yeye. Ukweli ni kwamba mtu uliyekuwa naye anajua jinsi gani unavyompenda, kumjali na kumuheshimu lakini bado alikuacha. Ki ukweli kumwonesha kumjali hakutakusaidia kwa sasa zaidi ya kumfanya akuchukie zaidi ya kumfanya akuchukie zaidi.
(e) Usichukie ukigundua yupo na mtu mwingine.
❤️Ni ukweli usiopingika kwamba watu wengi wanaumia sana wanapogundua kuwa mpenzi wake wa zamani anatoka na mtu mwingine. Watu wengi hali hii uwaumiza na kujisemea “kama nisipofanya kitu sasa mtu wangu atazama kwenye mapenzi na mtu mwingine. Hapa ndipo watu wengi wanfanya makosa niliyoyaeleza hapo juu kama kuomba msamaha, kumwambia ni kiasi gani bado anampenda au kukubali masharti yote atakayopewa.
Bado watu wengine uenda mbali zaidi na kujikuta unampigia simu na kumtumia sms siku nzima.
❤️Mbaya zaidi utakuta mtu anaamua kumchafua mtu ambaye anatoka na mpenzi wako wa zamani. Haya ni makosa makubwa cha msingi ndugu yangu jua kuwa kama mpenzi wako alikupenda kwa dhati na mahusianao yenu yalikuwa ya maana na yenye nguvu basi mahusiano atakayoanzisha yatakuwa ni ya mda mfupi tu.
❤️ Ni ukweli usiopingika kuwa kuingia kwenye mahusiano mapya ni njia watu wengi utumia kukabiliana na breakup(kuachana). Njia hii ni ya zima moto na kama mlipendana, hawezi kukusahau na lazima atapenda kurudiana na wewe siku moja.
❤️Kitu muhimu ni kutulia tu pindi mtu wako anapojaribu kutoka na mtu mwingine. Kwa vyovyote vile husimwambie mpenzi wako aachane na mtu aliyenaye kwa sasa. Ukweli ni kwamba atayeye moyoni mwake atakuwa na kidonda cha kuachana hivyo kuwa na mtu mwingine hakiwezi pona kwa urahisi.
NAJUA UTANIULIZA NIFANYEJE KAMA TAYARI NISHAFANYA MAKOSA HAYO.
❤️Nafasi bado ipo hata kama tayari ulishafanya baadhi ya makosa niliyoyataja baada ya kuachana. Usijali na kuumia sana kwani hata wataalamu wa saikolojia, matajiri na maprofesa uishia kufanya makosa hayo baada ya mfarakano.
❤️Ni kawaida kwa mwanadamu kukosea na waswahili usema tutajifunza kutokana na makosa. Kitu cha muhimu ni kujua kuwa makosa haya hayatakusaidia kurudiana na mpenzi wako na ukiweza acha kuyafanya.
🍏Daktari wa Mahaba🍏
May be an image of 2 people and people standing
All rea

Post a Comment

أحدث أقدم