Athari 10 za wivu katika mapenzi, mahusiano au ndoa.


Ikiwa unafikiria wivu si kitu, fikiria tena!  Kila mtu anajua kuhusu wivu, sawa? Labda umesoma madai kuwa wivu "mdogo" ni mzuri kwa mahusiano yako ya mapenzi au ndoa, au kwamba wakati mpenzi wako ana wivu, inamaanisha kwamba anajali sana. Ikiwa unapigana na wivu, labda unajua jinsi unavyoumiza na kuharibu mahusiano. Wivu sio mzuri kwa mahusiano yako, na sio mzuri kwako pia.

Ingawa mwenye wivu hutambua kuwa  wivu huo hauna manufaa, lakini ni moja ya vitu ambavyo bado huwezi kuacha kirahisi  Umeweza kujaribu jaribu njia zako binafsi za kuacha wivu. Pengine umejaribu kwa bidii kufuta mawazo ya wivu ambayo yanaingia ndani ya akili yako na kisha kujenga na kukusababisha kusema au kufanya mambo unayojuta baadaye.  Lakini ... Bado unaupata kiurahisi sana. Bado unamhoji mpenzi wako, au unajilinganisha na wengine kwa wasiwasi kwamba utasalitiwa na mwenza wako.  Wakati mwingine unapopatwa na vita kati yako na tabia mbaya kama wivu, fikiria madhara yanayoweza kutokea. Angalia mambo ambayo tabia yako ya wivu inakuzuia kupata kwa kuathiri aina ya ukaribu, uhusiano, imani na furaha na mahusiano unayotaka kwa mwenza wako.
Wivu unaweza ...

1. Hatarisha afya yako ya kimwili. Inasisitizwa kuwa wivu, na kinyongo cha muda mrefu inaongeza uwezekano wa kuwa na matatizo ya kiafya kama: shinikizo la damu, maumivu ya kichwa, maumivu ya mgongo, homa ya tumbo, vidonda na hata mashambulizi ya moyo au kiharusi!

2. Inahatarisha afya yako ya akili. Kuna aina fulani ya matatizo ya akili ambayo yanajitokeza kutokana na kuwa na wivu mkali sana. Lakini hata wivu wa kawaida unaweza kuwa na madhara kwa afya yako ya akili na kihisia. Unyonge na kushindwa kuchanganua mambo kwa haraka, hisia za woga, wasiwasi na kukosa usingizi ni mifano michache tu.

 3. Imani kwa mpenzi wako inapotea. Wivu husababisha kutoaminiana na mpenzi wako, na yeye anaweza kuanza kutojiamini pia. Mwenza wako hajui ni nini kinachokuweka katika hali hiyo. Yeye ataanza kuwa mwangalifu zaidi na wewe, kwa sababu unaweza kusema kuwa "uko sawa" dakika moja na kisha hasira za wivu zinakupanda dakika ijayo. Hii inafanya kuwa ngumu kwa mpenzi kukuamini pia.


4. Upungufu wa imani uliyonayo wewe mwenyewe. Hakuna shaka kwamba wivu huharibu imani yako mwenyewe. Unauliza hatima yako na uwezo wako wa kujua nini kinachoendelea kwa sababu ya picha ambayo wivu inakutengenezea kichwani.

5. Hufanya hali yako kuwa mbaya. Ikiwa upo kwenye mazungumzo na mpenzi wako au uko naye mahala, basi ile picha ya jambo uliloliona linalokupa wivu hukujia ghafla na kukufanya ukose amani

6. Unashindwa kufurahia mahusiano yako. Wivu hukurudiasha  nyuma  kwa kukukumbushia mambo ya wakati uliopita wa uchungu wa usaliti na tamaa. Huwezi kufanya maboresho katika mahusiano yako au kumfurahia mwenzi wako anachofanya kwa sababu kila unachoweza kuona ni yale ya nyuma yanayokuumiza.


7. Anzisha tena hoja ambazo wewe ma mpenzi wako  mlidhani mlishazimaliza. Hamtoweza kuzungumza vizuri na kukubaliana au kwa sababu akili yako ya wivu itarudi kwa kile unachofikiri kilichotokea - au kile unachofikiria mpenzi wako anakifanya, madhara yake - mnaanza upya tena na tena.

 8. Kuleta ugomvi na ushindani mkubwa zaidi. Unajua kujichukulia kuwa wewe ni zaidi kwa kuwa unafikiri wewe ndiye mkweli na wewe ndio uko sawa kushinda mwenzio kutazidisha ugomvi zaidi kati yako na mwenza wako.


9. Kuwa vigumu kuzungumza pamoja kila siku. Mawasiliano yanapungua wakati una tabia ya wivu.  Mada ya mazungumzo yanageuka kuwa ni mashaka na kujenga uadui kwa sababu huwezi kusikiliza kile ambacho mpenzi wako anasema.

 10. Itamfanya mpenzi wako kuwa na maswali mengi kichwani kuhusu mahusiano uenu. Kwa wakati mwingine, mpenzi wako atajiuliza kama mko serious au mnachezeana michezo na kupotezeana muda tu hii itamfanya kuanza kufikiria kukuacha.

 Hata kama mpenzi wako anakupenda sana, mashtaka yasiyo ya kweli na mambo ya kutokumuamini na kuhojiwa maswali mengi kunaweza kupunguza upendo wake kwako.

Post a Comment

Previous Post Next Post