Nimekuwa nikipata request za google kutoka kwa readers wa NESIMAPENZI wakitaka kusoma SMS za kutongoza, SMS za kimapenzi na SMS za mahusiano kiujumla. So leo nimeamua kuandika orodha ya SMS ambazo ukizitumia zitampendeza mwanamke na kutaka kuongea nawe milele.
Ok SMS tulizoziorodhesha hapa si SMS za kutongoza bali zinajaribu kuleta gumzo kwa mwanamke.
Psss! Kwa wale wasomaji wa blog hii kwa
muda najua wanajua jinsi ya kutumia SMS yeyote ile kuvutia mwanamke, hivyo kama wewe ni mgeni kwa NESIMAPENZI.com nakushauri usiendelee kusoma zaidi chapisho hili. Ingia hapa upate kujua sanaa za kutongoza kwanza.
Maswali 20 ya SMS kufanya maongezi yako na mwanamke yaendee kunoga kwa masaa
1. Ni kitu gani ushawahi kufanya, lakini hautafanya tena?
Swali kama hili litamfanya kufikiria sana. Swali hili laweza kufanya ujue mambo yake ya chini ya maji zaidi. Mwanzo labda unaweza kugundua ya kuwa kuna mambo ambayo mnagawa pamoja.
2. Tabia gani ya ufidhuli ambayo uko nayo?
Kila mtu ana tabia yake ya ufidhuli ambayo amezaliwa nayo. Hivyo swali kama hili litamfanya mwanamke kama huyu kujieleza zaidi hivyo kujiskia huru kuongea nawe zaidi na zaidi.
3. Rafiki yako wa dhati ni nani?
Rafiki wa dhati ni muhimu zaidi kama unataka mahusiano yako na mwanamke yafaane. Hivyo lazima ujipendekeze na kujihusisha na rafiki ya mwanamke unayemzimia ili kufunga mahusiano yenu yawe mazito. Unaweza kupanua mawazo yako kwa kumuuliza maswali kama alikuwa rafiki yake tangu lini? Ulimjuaje? nk [Soma: Sababu 11 za wewe kufanya mapenzi na rafiki yako]
4. Ni jambo/kitu gani ulichofanya kitambo ambacho ungetamani usingekifanya?
Kufanya makosa ni vigumu kuelewa na kukubali. Hivyo kumuuliza swali kama hili na akiweza kulijibu basi kunaashiria ya kuwa una nafasi kuu ya nyinyi wawili kuwa kitu kimoja.
5. Kitu gani unachoogopa zaidi?
Uoga ni kawaida. Ukijua uoga wa mtu kunakufanya uwe makini naye. Hivyo mwanamke akikuambia uoga wake anakupa ruhusa wa kutumia nafasi hii kumkinga na kumlinda mbeleni.
6. Sehemu gani hapa ulimwenguni ungetamani kuishi?
Swali hili linatoa nafasi kwa mtu kuwa mbunifu na kutoa hisia zake za ndani ya mwili. Pia swali hili linakupa nafasi kwako kujua matamanio yake hivyo unaweza kuchagua sehemu ambayo unaweza kumtoa out ama deti. Pia kuuliza hivi kunakupa kumjua zaidi mwanamke.
7. Ungependa kuchagua pesa au mapenzi?
Swali kama hili lafaa liwe mapenzi. Pili hivyo bila shaka mwanamke huyo tutamweka katika kategoria ya kuwa gold digger. [Soma: Jinsi ya kumtongoza mwanamke kwa kutumia macho]
8. Kumbukumbu ipi ya utotoni mwako unaipenda?
Kumbukumbu za utotoni humfanya mtu kuingiwa na furaha na tabasamu. Hivyo kumuuliza mwanamke swali hili kunatoa fursa ya kujua mambo ambayo yamekuwa yakimfurahisha kitambo.
9. Ni jambo gani la aibu zaidi ushawahi kufanya?
Mambo ya aibu humkumbusha mtu na kumfanya kucheka. Hivyo tumia fursa hii ya kumfanya mwanamke acheke.
10. Deti ya ndotoni mwako unapenda ingekuwa vipi?
Swali hili lina manufaa kwako. Hivyo akikujibu unaweza kutumia nafasi hii kupanga jinsi ambavyo utamtoa deti kama saprize. Utamwacha kwa giza.
11. Kitu gani ungependa kubadilisha maishani mwako?
Hakuna mtu anaridhika vile alivyo asilimia mia moja. Hivyo kujua udhaifu wake kutawafanya nyinyi wawili kuungana kuwa kitu kimoja.
12. Nani amekuwa mshawishi mkuu katika maisha yako?
Swali hili litakufanya kumjua zaidi katika maisha yake. Ukiskia anakwambia kuwa mshawishi wake ni Agness Masogange ama Corazon Kwamboka basi fahamu mwanamke aina hii anapenda maisha ya hali ya juu. Lakini ukimskia akikutajia mamake huyo ni wa kumpeleka nyumbani akawaone wazazi wako haraka sana. [Soma: Sifa za mwanamke mzuri]
13. Ni vitu gani ulikuwa ukipenda kufanya ukiwa utotoni na ungependa kufanya sahizi?
Swali kama hili ni kama kuufungua moyo wake kupata kujua maisha yake ambayo anayaota kufanya. Unaweza kuchukua nafasi kama hii kutumia kama kigezo cha kumfurahisa wakati wowote. Mfano kama anapenda kubembea ama mfanano wa hii unaweza kumridhisha. Ilimradi tu umwone na furaha.
14. Kitu gani unachukia katika deti?
Swali hili litakuwa sehemu ya pili ya swali la #10 hivyo kukupa nafasi ya kujipanga ili uepuke makosa madogo madogo ya kudeti.
15. Maisha yako ya mbeleni unataka yaweje?
Kama unaye SMS naye ni mwanafunzi unaweza kumchokora akili yake uone mambo anayofikiria ama kazi anayotamani mbeleni. Kama unayem Sms anafanya kazi, jaribu kujua maisha yake ya usoni anayapanga vipi. Mfahamu iwapo anataka kuwa sehemu moja ama ana matamanio ya kuendelea mbele kimaisha.
16. Je uko karibu na familia yako?
Swali hili linaweza kuwa na utatanishi kiasi. Unaweza kujua tabia ya mwanamke kwa urahisi zaidi iwapo utauliza swali kama hili. Akisema hana uhusiano wa karibu na wazazi wake basi bila shaka kuna tatizo flani.
17. Filamu gani imekushawishi zaidi?
Ok. Filamu huwa zinaonyesha tabia za mtu. Hivyo akikwambia filamu flani ya mapenzi, ya kupigana ama ya ucheshi utajua msimamo wake kiurahisi. [Soma: Leonardo DiCaprio atufunza kutongoza mwanamke chini ya dakika 3]
18. Sehemu ambayo unaiona salama zaidi maishani mwako ni wapi?
Kujiskia salama kwa mwanamke ni jambo muhimu zaidi kwa maisha yake. Hivyo inaweza kuwa popote pale. Labda inaweza kuwa ufuoni ama hata nyumbani anakoishi.
19. Ni kitu ama jambo gani ambalo ungependa kufanya kabla hujafa?
Kila mtu kuna kitu ama jambo flani anapenda kutimiza maishani. Hivyo swali hili litamfungua zaidi. Pia swali hili unaweza kulitumia kwa manufaa yako kwani unaweza kumsaprize mwanamke kwa jambo ambalo ana matamanio.
20. Malengo yako unayopania kutimiza ni yapi maishani?
Swali hili linarudia lile la #15 lakini linatoa mtazamo ya maisha yake ya ujumla. Ni vizuri kutambua iwapo mwanamke unayem Sms ama kuchat naye analingana na tabia unazotaka.
Ok hizi ni baadhi ya Sms ambazo unaweza kutumia mwanamke kuleta maongezi ambayo yatakzunguka siku nzima.
NB: Kila swali ambalo utakuwa ukitumia hapa hakikisha ya kuwa unapanua mawazo ya kuleta maswali zaidi kabla hujauliza swali la pili.
Psss! Usisahau kubookmark hii page kwa browser yako ili kurahisisha usomaji wakati mwingine
Post a Comment