LOVE

 


Suala la wanandoa kutokuwa waaminifu kwenye mahusiano yao ni suala mtambuka na limekuwa likiongelewa sana na watu wengi. Sababu mablimbali zimekuwa zikitajwa kuwa chanzo, nyingine ni za kweli na nyingine ni zakufikirika tu.


Leo nimeamua kuja na sababu zinazotokana na tafiti za wanaume kutokuwa waaminifu kwenye mahusiano na ndoa. Ikumbukwe kwamba sababu za wanawake kutokuwa waaminifu hazifanani moja kwa moja na sababu za wanaume, na hata kitendo chakutokuwa mwaminifu kwenye ndoa kwa mume au mke pia huathiri ndoa husika katika uzito tofauti. Hii ni kutokana na sababu za kiasilia, kiuumbaji, kiji


Sababu



1. Utupu au upweke ndani ya moyo wa mwanaume


Pamoja na kwamba wanaume huonekana wakiwa jasiri sana kwa nje ila ieleweke kwamba ni viumbe dhaifu ndani, ni viumbe wasioweza kuvumilia upweke ndani yao, wakati wote hutamani kuwa karibu na mwanamke hata kama akiwepo karibu hawaelewani mara kwa mara. Maranyingi kwenye mahusiano unakuta mwanaume ameoa au ana mpenzi na kuna mambo yanaendelea ambayo yanasumbua mahusiano yao, ukaribu unapokosekama mwanaume huanza kujihisi upweke ndani yake na hapo inanyanyuka kiu ya kutafuta mtu wakuondoa upweke ule.


Inasemekana kwamba wanaume wengi huchepuka au kuanza mchakato wa kuchepuka kunapokuwa na tafrani kwenye mapenzi au ndoa, ni kwanini? Sababu ni kwamba ule ugomvi umeleta baridi moyoni na nafsini kwa mwanaume na hawezi kustahimili upweke huo ndani yake kwahiyo anatafuta faraja haraka sana.


2. Uasili wa kiu kubwa ya mwanaume katika tendo la ndoa


Kiaasili na kibaiolojia mwanaume anakiu kubwa na utayari wa kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, mwanaume wa kawaida anaweza kutamani kufanya tendo la ndoa hata kila siku, na wengine hata marambili kwa siku kama kila kitu akilini na katika afya yake ni sawa. Utayari na uwezo huu ni tofauti sana kulinganisha na wanawake ambao kama akifanya tendo zuri la ndoa na hamu yake ikitoshelezwa basi anaweza kukaa muda fulani bila kutamani tena.




3. Kubadilika kwa uzuri, urembo na maumbile ya mke


Mara nyingi ninapoongea na wanawake huwa ninawaambia kwamba mume wako anakupenda uwe vile alivyokupenda alipokutana nawewe, mabadiliko yoyote ya ziada kutoka kwenye ile hali iliyompa hamasa awali yanaweza kuigharimu ndoa yako. Wanaume ni watu wenye kuhamaki au kuwa makini kwenye umbo, umbile na muonekano wa mpenzi wake kwasababu kwa asili mwanaume huvutiwa zaidi na akionacho, mwanaume hufungulia milango ya hisia inayohusu tendo la ndoa kupitia anachokiona zaidi kuliko vitu vingine vyote.


4. Kuchangamkia fursa ya kupata tendo la ndoa jepesi


Kwasababu wanaume ni watu wanaopenda tendo la ndoa mara kwa mara, na kwasababu wake zao hawako tayari kutimiza kiu hii mara kwa mara kulingana na uhitaji, wanaume wengi huchangamkia fursa pale wanapokutana na uwezekano wakupata tendo la ndoa kirahisi na kiwepesi.


5. Kisasi “revenge”


Mara nyingi wanaume hutumia kitendo cha kutoka nje ya ndoa au nje ya mahusiano kama fimbo ya kulipiza kisasi kwa maumivu au hasira yoyote aliyokuwa nayo dhidi ya mpenzi au mke wake. Kwa mfano, wanaume wengi nilioongea nao binafsi, hususani wale ambao walikuwa wanalalamika kuwa mke wangu haniheshimu, mke wangu ananidharau, mke wangu hanisikilizi, mke wangu anafanya hivi au anafanya vile, wengi baada ya kuongea au kulalamika kwa muda mrefu pasipo kuona mabadiliko baadaye waliamua kuanza ku “cheat”.




6. Mkanganyiko wa matarajio ya mwanaume


Wako wanaume wengi ambao kabla hawajaoa walikuwa na shauku kubwa kwa wake zao, walikuwa na matamanio au matarajio makubwa kwa wake zao. Wengine walioa wake zao kwasababu ya maumbo mazuri na yakuvutia, wengine ni aina ya familia wanawake hao walizotoka, wengine walioa wakitegemea huyu mwanamke ni mcha Mungu sana, au uliwahi kusikia habari zake nzuri kwa watu na ukatamani sana kuwa naye maishani na mara baada ya kuingia kwenye ndoa bahati mbaya yale mambo uliyokuwa unakiu nayo sana na kuyatarajia unakuta sio yalivyo.





7. Kutokupevuka


Wapo wanaume kwenye ndoa hususani wenye umri usio mkubwa sana wamekuwa wakiripotiwa kuchepuka mara kwamara kwasababu tubado hawajafahamu umuhimu wa ndoa ili kuithamini, wameoa lakini bado fikra zao zinatawaliwa na marafiki, hawawezi kujisimamia wenyewe, mtu anaweza kukaa baa na marafiki hadi usiku sana bila kujali kwamba ana mke na watoto. Huko nje usiku ndipo fursa za uchepukaji huzaliwa. Wapo ambao wamechelewa kupevuka kutokana na aina ya malezi waliyolelewa na wazazi wao “spoilt children”, hawa hushindwa kuiheshimu ndoa na mke hatakama mke alalamike vipi.


8. Kujifariji kwamba kila mtu anafanya


Wapo wanaume wengi walioonyesha kuchepuka kwasababu tu ndani yao walikuwa wanakosa umaana wa kuwa waaminifu kwasababu wanaona hata wale watu ambao wao waliwaamini kwamba labda wanaweza kutochepuka na wao pia walichepuka, sasa mtu anasema kumbe kila mwanaume anachepuka, basi yanini kujibanabana wakati namimi ninahamu na fursa inaruhusu.

Post a Comment

Previous Post Next Post