Ukinimiss nipigiee
Mbio nikukimbilie
Nije nikukumbatie
Na uzio tuyajengee
Nakupenda wangu wa ubani




























Miundombinu imara kwa pamoja tuijenge 
Kurahisisha msafara ili mbele tusonge 
Tupite kwa furaha na waone donge
Ni iliyoje raha sana nisiongee
Kila king'aacho chatakiwa kiundwe
Na wajuee wangu mwandani




















Na kama shule tutaijenga
Tukajifunze mapenzi yale ya wahenga
Historia ya mapenzi yetu tutatunga
Ije kuwasaidia wa mapenzi wahanga
Kwa ujuzi wa mahaba tutaringa
Kwenye top one tutie nanga






























Hospital ya mahaba mkazo naitilia
Daktari nimebobea mapenzi kukutibia
Tiba za kila aina kuhakikisha unapona nitakupatia
Ondoa shaka nimejipanga vyema nakuhakikishia
Ni wewe my number one




Sekta ya kilimo kwa pamoja tutashirikiana
Na pia sekta ya michezo tena ya kila aina
Nipo tayari kujitoa kwako kwa kila namna
Bila ya kusahau sekta ya utalii wa mapenzi nitakuwa kivutio sana
Najivunia uwepo wako yangu mboni

































Huduma za kijamii zote nakuhakikishia
Na hata pia sekta ya uchumi nitajitahidi kuhakikisha hautoumia
Sera yangu haina ushindani jimbo limepata mgombea najisifia
Lete marekebisho niongeze ibarani kama kuna mapungufu hujayaridhia
Nilokupenda ni wewe tuu mwengine sioni






























Nakupenda wangu mpenzi 
Natuma Cv kwanye serikali yako ya mapenzi
Tadhali nipe kazi tushirikiane ujenzi
Sitokuangusha nakuhakiishia uzalendo na ulinzi


























BY LATIFA MCHENGULE
Jiunge katika group hapo chini

Post a Comment