Shukran za dhati zije kwako sweetdarling kwa kunipa nafasi moyoni mwako







Wapo wengi walitamani kupata nafasi kama hii kutoka kwako my sweetheart ukanichagua mimi pekee na kunikabidhi funguo ya moyo wako













Naahidi kuutunza moyo wako na frame ghali nitaujengea laaziz kulienzi penzi lako







Sio siri nakupenda sana babe nikifumba na kufumbua macho mpenzi ninahisi uwepo wako







Nachotaka kukuambia nashukuru sana kwa nafasi hii adhwimu uliyonigea
Kwa mapenzi mwanana moyo wako nitakutunzia kwa hakika fursa kama hii ni ghali kuipata wengine wanaingojea







Akhsante sana mimi ni wako usinionee aibu chochote cha kudumisha penzi letu kuniambia
kuwa huru CEO wa moyo wangu mtumishi wako nipo tayari majukumu kuyapokea







Akhsante sana mpenzi nakupenda na nitazidi kukupenda zaidi ya sana







BY LATIFA MCHENGULE
Jiunge katika group kwa link hapo chini

Post a Comment