❤️❤️SMS TAMU ZA❤️ KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO❤️



Uzuri wa usiku si giza lifunikalo dunia wala si kimya kinachotawala mazingira bali ni njozi njema zenye maono na matarajio yenye mafanikio. Nakutakia ucku mwema
°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°
Kama jicho langu halija kuona basi moyoni daima nakukumbuka na ikiwa dua zangu hazijakulinda basi mungu daima
atakulinda,nami cna budi kukutakia usiku mwema.
°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°
Upendo ni tiba maradhi hukimbia. Salamu ni shiba biriani yazidiwa. Kukumbukana ni haiba nuru hutuangazia. Kwa furaha na mahaba sichoki kusalimia. Usiku mwema
•·.·°¯·.·•*•·.·°¯·.·•
Salio la macho yako halitoshi kuendelea kuona kwa sasa tafadhali tandika kitanda na ulale,kwa maelezo zaidi subiri usingizi ukolee uote ndoto nzuri. usiku mwema!
•·.·°¯·.·•*•·.·°¯·.·•
ni usiku tulivu wenye hali ya hewa saafi na usingizi wa amani ukishika hatamu kuzisafirisha fikra za binadamu katika ndoto! najua umechoka na pilikapilika za mchana ,jua na makelele na kila aina ya mwingiliano wa sauti ,ni wasaa mzuri sasa wakupumzisha mwili na akili yako.amua kumsamehe aliyekuudhi mchana wa leo na pia kumbuka ulipokosea leo ili kesho usirudie,lakini pia jipongeze kwa mafanikio ya mipango yako,fumba macho uikaribie nchi usiyoijua.usiku mwema
•·.·°¯·.·•*•·.·°¯·.·•
lala ulale vyema na upoe moyo wako,lala ulale salama utulie roho yako,lala usingizi mwema upumzishe akili yako,akujalie
karima zitimie njozi zako.usiku mwema
•·.·°¯·.·•*•·.·°¯·.·•
Mpenzi tambua wewe ndiye sababu ya huu usingizi, najilaza kwa pozi nikiamini tutakutana kwenye njozi, njozi za kulienzi letu penzi, Nakupenda mpenzi, gn mwaaah…!!

Post a Comment

Previous Post Next Post