Kila mwanaume ana kipawa cha kutongoza mwanamke yeyote kwa kutumia matamshi yake. Huu ni uwezo ambao wanaume wamebarikiwa nao. Tatizo ni kuwa kipawa hiki hakiji kwa wakati mmoja kwa kila mwanaume. Wengine inaweza kuwachukua miaka mingi hadi kujigundua na wengine huwa na kipawa hiki tangu utotoni.
Well, kile ambacho tunajua ni kuwa itafikia wakati flani kipawa hiki lazima kije chenyewe tu. Aidha miaka ya ishirini ama miaka ya thelathini au hata miaka ya arobaini kuendea juu.
Je, utahisi vipi kama kipawa hiki utakivumbua sasa hivi? Kama uko tayari kuvumbua kipawa chako cha kutongoza mwanamke ingia >>hapa<<
Somo la leo ni kuvumbua kipawa chako cha kutongoza mwanamke kwa kutumia maneno. Maneno ni njia moja wapo ya nguvu ya kukuwezesha kufaulu kumpata mwanamke yeyote yule. Ukichanganya maneno pamoja na vitendo utaongeza nafasi yako zaidi ya kumpata mwanamke wa ndoto yako.
Fuata mbinu hizi ambazo tumeziorodhesha ili uweze kutumia kipawa chako ili uweze kumtongoza mwanamke yeyote yule.
#1 Punguza sauti yako unapoongea.
Wakati ambapo unamtongoza mwanamke, hakikisha ya kuwa sauti yako inakuwa ya toni ya chini. Hupaswi kumpigia makelele mwanamke ili aweze kukusikia. La kufanya ni kuhakikisha ya kuwa sauti yako inakuwa ya chini kiasi cha kuwa ni yeye pekee anaweza kukusikia. Hii itatoa nafasi ya mwanamke kumakinika na pia kuweza kumfanya ajaribu kukusogelea ili aweze kuyasikia maneno yako matamu. [Tazama: Mfano mzuri wa kuzungumza kwa sauti ya chini]
#2 Msogelee katibu lakini usimguse.
Hapa utajaribu kuleta mazingira ya mapenzi. Msogelee karibu lakini usimguse. Jaribu kumaintain ukaribu na yeye lakini usijaribu kumgusa. Wewe unalotakiwa ni kuishukisha sauti yako. Msogee karibu kiasi cha kuwa unauondoa ule ukaribu ambao marafiki wanaweza kuwa nao.
Sasa mwambie kila kitu ambacho ulikuwa unataka kumwambia askie. Njia hii itamfanya ajihisi spesho na pia kuona maneno unayomwambia yana umuhimu kwake.
#3 Pata kumjua mwanamke kiundani.
Wakati unapomtongoza mwanamke, jambo muhimu zaidi ambalo unapaswa kulifanya ni kumjua mwanamke huyu kiundani. Huku kutakupa uwezo wa kutumia maneno kadha wa kadha ili uweze kumtongoza zaidi. Jaribu kufanya bidii kujua mambo anayopenda, anayochukia, vitu anavyotamani na kadhalika.
#4 Muulize maswali ya kusisimua.
Wakati unapomuuliza maswali ya kumsisimua, hakikisha ya kuwa hauvuki mipaka. Ongea mambo sahili ambayo hayatamfanya aanze kukushuku. Usiingie ndani kumsisimua sana bali gusa tu juu juu. Mfano unaweza kumuuliza maswali kama ‘wapenda kufanya nini wakati ukiwa free?’ Huku kutampa fununu ya kuwa labda unataka kumtoa deti ama unataka kuspend muda mwingi na yeye. Lakini pia unapaswa kuwa mjanja asifikirie ya kuwa unataka kumpeleka chemba. [Download: Kitabu cha mistari ya kumwambia mwanamke]
#5 Jaribu kadri iwezavyo usimsifie maumbile yake.
Hapa kuna changamoto nyingi ambazo wengi huanguka. Badala ya kuongea kuhusu urembo wake ama tabasamu lake, hakikisha ya kuwa unahepa mada hii na badala yake msifie kwa ubunifu wake, ucheshi wake, ujanja na mengine kama haya. Nasema hivi kwa kuwa wanaume wengi hukimbilia kumsifia mwanamke, jambo ambalo ashazoea kuliskia na amechoka nalo. So utakuwa na nafasi nzuri ya kumuwini iwapo utaamua kutumia sifa za hulka yake badala ya maumbile yake.
#6 Kuwa mcheshi.
Tumekuwa tukiongelea hili tangu jadi. Uwezo wako wa ucheshi ni silaha kuu ya kuwinda wanawake. So ukiwa unataka kufaulu kumtongoza mwanamke kwa njia iliyo sahihi, tumia ucheshi wako na bila shaka utafaulu haraka sana.
#7 Mhimize na umpatie sapoti ya vitu anavyotamani kufanikisha.
Baada ya kuifuata hatua ya tatu tuliyoieleza hapo juu, bila shaka mwanamke atakueleza mambo yake mengi, mengine muhimu na mengine yasiyokuwa na umuhimu. Sasa ukitaka kufaulu kumtongoza mwanamke kwa njia thabiti basi hakikisha ya kuwa unamhimiza kuendeleza ndoto zake. Kama anataka kuwa mtu flani katika maisha yake basi unapaswa kumhimiza afuate ndoto yake.
Wanaume ambao hupuuza kipengele hiki mara nyingi hupata taabu ya kufanikisha ajenda zao za kumnasa mwanamke ndio maana kila siku utapata wananijia kwa inbox wakitaka niwafafanulie zaidi jinsi ya kumuwini mwanamke ilhali tayari mbinu ziko nyusoni mwao.
#8 Kuchanganyikiwa.
Hii ni mbinu nzuri ambayo unaweza kuitumia ili kumnasa mwanamke kwa njia ya haraka. Mbinu hii inatumika pale wakati mwanamke anazungumza kisha umemkodolea macho bila kuangalia kando. Kisha baada ya madakika unamwambia, “Samahani sikupata kuelewa umesema nini, umenichanganya kiasi.”
Mbinu hii inampa mwanamke confidence ndani yake akiwa na fikra za kuwa umbo lake limekuchanganya. Mbinu hii hufanya kazi asilimia mia.
Well, hii ni miongoni mwa mbinu ambazo unaweza kutumia ili kuweza kumtongoza mwanamke kwa kutumia kipawa chako cha maneno.
SAMBAZA:
Post a Comment