Maneno 100 Ya Kumwambia Mwanamke Ili Moyo Wake Usisimke


Hivi yule mwanamke unayemtongoza ushamwambia maneno mangapi matamu na akakuambia kwa upole, “Nakupenda mpenzi wangu”. Iwapo hujawahi kutamkiwa maneno kama haya na mwanamke kwa njia ya upole basi itakuwa yale maneno unayomwambia hayatosheki.



Mwanamke anapenda kuona kuwa unamfukuzia. Anataka kujua iwapo unamwona ni mrembo na kuvutia au la. Wanawake ni viumbe tofauti na huchagua maneno. Unaweza kuwa kila siku unamrushia mistari ama voko ambazo umekuwa ukizihifadhi kumbe kwake haoni chochote.

Kabla hatujaendelea, sababu ya kuandika post hii ni kuwa kuna rafiki yangu katika mtandao wa Facebook amekuwa akiniandama akitaka nimpe mistari angalau mmoja ili aweze kumzuzua mpenzi wake. Well, kwa hili tulikaa na paneli yetu ya Nesi Mapenzi na tukaamua kuweka maneno 100 ambayo bila shaka yatamridhisha mwanamke yeyote. Zama nasi. [Soma: Sms nzuri za kumtumia mwanamke baada ya kupewa namba]

Maneno matamu ya kumwambia mwanamke

#1 Nakumbuka ile siku ya kwanza ambayo macho yangu yalipokuona

#2 Nilijua kua wewe ni wangu kuanzia ile siku

#3 Unavutia

#4 Yaani niko in love na wewe

#5 Nahisi mbaya kwa wale wanaume wote mabwege ambao hawatoweza kuwa na wewe kamwe

#6 Kukutana na wewe kumefanya maisha yangu kukamilika

#7 Finally nimejua maana ya mapenzi baada ya kukujua

#8 Napenda marafiki zangu, lakini wewe ni maisha yangu

#9 Kama ningeweza kufanya mtu awe maishani mwangu milele basi ningekuchagua wewe

#10 Nafanya kazi siku nzima ili nifike nyumbani kwa ajili yako

#11 Tabasamu lako linasisimua moyo wangu

#12 Una kitu ndani yako ambacho kina fanya kila kitu kuwa sawa

#13 Wewe ni kila kitu kwangu

#14 Umekamilika

#15 Ni vipi nimebahatika hadi nimekupata wewe

#16 Nashukuru kila siku ambayo napata kuangalia macho yako

#17 Mimi siko romantic, lakini kwa sababu yako nimeamini kila kitu kinawezekana

#18 Wewe ni kama hewa kwa moyo wangu, siwezi kuishi bila wewe

#19 Unapendeza hata kama umekasirika

#20 Nakupenda si kwa ajili ya urembo wako bali kwa sababu wewe ni mrembo

#21 Maisha yangu yalikuwa ya rangi nyeupe na nyeusi lakini sasa ni rangi ya upinde

#22 Unakimbia kwa akili yangu siku nzima

#23 Nataka nispend maisha yangu yote kukufanya uwe na furaha

#24 Sikuwa naamini kuwa kuna kitu kinaitwa upendo wa dhati hadi ile siku tulikutana

#25 Nataka tuwe pamoja hadi ile siku tutakuwa wazee

#26 Kama watoto wetu watafanana na wewe basi watapendeza

#27 Sikuwa naamini kama ukamilifu unapatikana katika hii dunia hadi ile siku nilipokutana na wewe

#28 Napenda jinsi unavyonipenda

#29 Tufanye hivi

#30 Kusema nakupenda kutapungua ladha lakini mapenzi yangu kwako hayataisha

#31 Natumai siku yako ilikuwa njema kama venye uko

#32 Wewe ni rafiki yangu wa dhati na mpenzi wangu bora. Yote ikiwa imewekwa mahali pamoja

#33 Nataka kukusaidia kuosha vyombo

#34 Kutulia na wewe ni kitu ambacho nimekuwa nikingojea maishani

#35 Nikiangalia macho yako kile kitu ambacho naona ni moyo wangu

#36 Unamaanisha kila kitu kwangu katika hii dunia

#37 Vitu havifurahishi iwapo hauko karibu

#38 Kuna wakati mwingine yaani huwa naona kama unazichukua pumzi zangu

#39 Wakati mwingine nashindwa kujizuia kuangalia uso wako wa kupendeza

#40 Unanifanya nacheka kwa njia ilio raha

#41 Sikudhani kama naweza kuhisi hivi maishani mwangu

#42 Nahisi kana kwamba maisha yangu yote yamenileta ili niwe na wewe

#43 Chukua mkono wangu na wala usiuachilie

#44 Kuwa mpole, umeuteka moyo na roho yangu milele

#45 Hakuna mtu mwingine, ni wewe tu ndie naweza kuwa naye

#46 Kama kungekuwa na nafasi ya kurudia tena, bado ningebaki kukuchagua wewe

#47 Tabasamu lako si la kawaida kwa kuwa linafanya moyo wangu kusimama

#48 Kile ambacho nataka kufanya ni kuwa mwanaume bora zaidi hapa duniani kwa ajili yako

#49 Unafanyaje hadi unaweza kuwa kuwa mkamilifu kirahisi?

#50 Akili na urembo umechanganywa kwako. Wewe ni zawadi bora zaidi hapa duniani

#51 Kama nahitaji mtu, huwa nakufikiria wewe wa kwanza

#52 Tabasamu lako linanifanya nitabasamu

#53 Ni lini nitapata kukuona zaidi?

#54 Waonaje mahusiano yetu tuyapeleke level nyingine

#55 Nilidhani nitakuwa pweke milele lakini umebadilisha kila kitu

#56 Nakuhitaji katika maisha yangu

#57 Nashukuru kwa kila kitu umenifanyia

#58 Siku yangu haiwi sawa kama haijaanza na wewe

#59 Nahisabu kila sekunde hadi ule wakati utakuwa kando yangu

#60 Uko sawa kwa kila kitu

#61 Hakuna kitu kwako ambacho sikipendi

#62 Nilidhani kuwa nimependa kitambo, lakini sasa najua kitu cha ukweli ni kipi...ni mimi na wewe

#63 Kama utaniruhusu basi nitahakikisha kuwa nimekufanya uwe na furaha milele

#64 Nakupenda hata kama wakati mwingine nashindwa kukueleza

#65 Nisamehe kama kuwa siko kama vile unavyotarajia kila siku

#66 Nikifikiria maisha yangu ya usoni lazima uwe ndani

#67 Wewe ni dira yangu ya kufika nyumbani

#68 Usiwe na wasiwasi kuhusiana na chakula cha jioni. Kila kitu nimeshughulikia

#69 Unapendeza kama dhahabu leo

#70 Sikulala jana usiku. Nilikuwa nikiangalia jinsi ulivyo mrembo

#71 Nataka niwe mwanaume wa ndoto yako kama vile ulivyo ndoto yangu

#72 Unanifanya niwe mwanaume bora zaidi

#73 Nilikuwa naota usiku na nikaamka. Niligundua siko ndani ya ndoto bali naishi ndotoni na wewe

#74 Hakuna mtu hapa duniani ambaye ananiweza kama wewe

#75 Wewe ni rafiki yangu wa dhati mpenzi

#76 Nitapotea bila wewe

#77 Kila mtu katika hii dunia naweza kumtenga, lakini kwako siwezi sababu sitatoboa

#78 Mapenzi yako kwangu ni muhimu kuliko hewa

#79 Nataka uwe ubavuni mwangu katika uhai wangu

#80 Kukupata wewe kulikuwa kitu bora zaidi katika maisha yangu

#81 Natumai unafurahia siku yako, kukufikiria wewe kunaifanikisha siku yangu vyema

#82 Nataka kukufanyia jambo zuri leo usiku

#83 Uko mrembo, mzuri na unavutia kwa pamoja

#84 Bado unachukua pumzi zangu hata baada ya miaka hii yote

#85 Nakupenda zaidi kila siku

#86 Maisha yangu yalianza ile siku tulikutana. Ni kama nilifungua macho kwa mara ya kwanza

#87 Unafanya maisha yangu ya usoni kuwa bora

#88 Mapenzi yako kwangu ndio mwisho wangu

#89 Siwezi kuwepo bila wewe

#90 Waonaje tuwe mimi na wewe milele

#91 Unajua jinsi unavyonifanya kuwa na furaha maishani?

#92 Kama ningekuwa na uwezo wa kufanya ulimwengu wote upotee ili nibaki mimi na wewe pekee

#93 Sikudhania mtu kama wewe angeweza kupenda mtu kama mimi

#94 Unanishangaza kwa njia tofauti kila wakati na kila siku

#95 Yaani ungejua venye nakupenda

#96 Wewe ni mrembo ndani na nje

#97 Huwa sisemi nakupenda vya kutosha, lakini ni kila wakati

#98 Ningekwambia kuwa wewe ni kiumbe kamili lakini pia sifa hii haingekutosha

#99 Kama singekupata basi singekuwa na raha kama nilivyo sasa

#100 Nataka kufanya kila siku ambayo tuko pamoja kuwa kumbukumbu ya milele.

Haya ndio baadhi ya maneno ambayo unaweza kutumia kwa mpenzi wako ili avutiwe nawe. Si rahisi kumfanya mwanamke akupende asilimia 100 lakini ukiwa na kitu cha kumweleza hisia zako basi utafanya mahusiano yenu kuwa na nguvu zaidi.

Post a Comment

Previous Post Next Post