1. Kuwa tofauti
Hii ni mbinu muhimu zaidi ambayo unafaa kuiweka viganjani mwako. Kama wataka mwanamke yeyote, basi unapaswa uwe tofauti na wanaume wale wengine wote ambao wanamfukuzia.
Itakusaidia zaidi kama utafanya utafiti wa kina kwa mwanamke aina hii. Lazima ujue mambo ambayo anayapenda maishani mwake. Mfahamu vizuri kama ni mwanamke anayependa kujua mambo mapya ama ni mwanamke mwenye aibu. Pia mfahamu kama ni mwanamke anayependa kutangamana na watu ama ni wale wapole. Kimsingi hakikisha unafanya utafiti wa ndani zaidi kumhusu ili hio siku mtakutana ama unapoongea naye hatoboeka na wewe.
Kama utaamua kutofanya utafiti wowote kumhusu na ukaamua kwenda direct moja kwa moja kwake, basi fahamu ya kuwa wanawake hawapendi wanaume ambao wanaboesha, na ambao wanatabirika kirahisi. Ok. Mbona usijaribu kuvalia nguo ya rangi nyekundu? Yeah. Kulingana na utafiti wa kisayansi, wanawake huvutiwa sana na wanaume ambao huvalia rangi nyekundu. Wanawake hupendezwa na wanaume tofauti na wenye kuvutia.
Kumbuka- si lazima uoekane bora zaidi; bali tofauti.
2. Mwonekano wako
Tofauti na tamaduni za tangu jadi, si lazima mwanamke apendezwe na mwanaume mrembo wa kuvutia ndipo atoke deti na yeye. Ijapokuwa kuvutia na kuwa na miraba minane ni nyongeza katika sekta ya dunia ya kudeti, si muhimu sana kama inavyopigiwa kamsa. Vivyo hivyo, ni muhimu sana kama utaubadilisha mwonekano wako ili uweze kumvutia mwanamke unayeazimia kumfukuzia. [Soma: Mbinu za haraka za kuujeuza mwonekano wako]
3. Jenga uzingiti wa hisia
Kama wataka kujua njia rahisi ya kumfanya mwanamke akupende kwa uharaka, jenga uzingiti wa hisia na yeye (ok. wengi wanaogopa mbinu hii kwa kuwa ni rahisi kuwekwa katika kategoria ya friend zone) lakini kama utamfanya mwanamke kuwa rafiki yako kabla kumwambia azma yako, utakuwa na nafasi kubwa ya kumjua ndani na nje na kila kitu kumhusu, kutumia muda wako mwingi na yeye na pia kumfanya ajiskie huru akiwa na wewe. Bydaway nani hajui kama rafiki yako anapaswa kuwa mpenzi wako? [Soma: Sababu za lazima unafaa kufanya mapenzi na rafiki yako]
4. Ongea (tumia viini macho)
Kwa kawaida huwa ni vizuri zaidi iwapo utaanza approach ya kwanza kumtongoza mwanamke unayemzimia kabla ya yeye kuchukua hatua. Pia ni vizuri kujua mada ambazo zitamfanya yeye kukupenda bila ya yeye kuelewa ni kwa nini. Maongezi yako hapa unafaa kuyafanya ya KUZIMU na pia matumizi ya maongezi ya viini macho. [Soma: Matumizi ya viini macho kumsuka mwanamke]
5. Kuwa Juma Nature
Wanawake wengi wangependa kudeti mwanaume ambaye anamaisha yake binafsi kando na dunia ya kudeti. So iwapo utamwonyesha mwanamke ya kuwa wewe una kazi zako nyingi binafsi wakati wako wa uhuru utamwashiria mwanamke ya kuwa hutaambata kwake na hutotaka kuutumia muda wake mwingi kwako. Pia hii itaashiria ya kuwa umekomaa na una maamuzi na malengo yako binafsi maishani na kuwa si rahisi kwako kumuacha.
6. Tangamana
Wanawake wengi huwa wanapenda kutangamana, hivyo itasaidia pakubwa iwapo pia wewe unapenda kutangamana. Mwanzo uzuri wa kutangamana ni kuonyesha ishara kwa mwanamke ya kuwa maisha yako hayaboeshi hivyo itakuwa rahisi kwa mwanamke kukupenda. Usione haya ama aibu, tangamana na marafiki zake, familia yake ili upate kuwajua zaidi na pia kukupa alama za ziada za kupendekezwa. [Soma: Jinsi ya kujifundisha kukutana na wanawake wapya]
Mwisho ni lazima ujue mbinu tofauti tofauti za kunoa makali yako ya kumfanya mwanamke akupende. Posts nyingi humu ndani zitakupa mwongozo wa wewe kufanisha azma yako kwa urahisi sana.
Post a Comment