Orodha ya SMS za mapenzi za kumiss mpenzi wako"




"Kwa mpenzi wangu, wewe ni mwanamke mrembo zaidi kuliko kiumbe chochote katika maisha yangu. Nakupenda zaidi ya kitu chochote ama yeyote. Ndoto yangu ni kuwa penzi letu litaendelea kuwa na nguvu kadri siku zinavyosongea.


" Wewe ni mpenzi wangu na umenipatia sababu milioni kwa mimi kutabasamu kila siku.


"Kwa sababu ya penzi lako, mpenzi wangu, naweza kuukwea mlima mrefu zaidi na pia kutatua matatizo makubwa zaidi. Penzi lako kwangu linayapa maisha yangu sababu za kufanikiwa.


"Nikiwa na wewe ubavuni mwangu na penzi lako likizunguka moyo wangu, naweza kufanikiwa na chochote. Unanipa nguvu na nishati ya kukabiliana na chochote. Nakupenda kwa moyo na roho yangu.


"Bila penzi lako katika maisha yangu, maisha yanakuwa ya upweke na kiza. Wewe ndie unayeleta mwangaza na rangi ya upinde kwa maisha yangu, hata kama ni nyakati za mawingu. Asante sana mpenzi wangu.


"Furaha inapulizwa katika maisha yangu wakati unaponitabasamia. Unapoongea, sauti yako ina nguvu ya kunipeleka sehemu ambayo kuna upendo na amani.

Post a Comment

Previous Post Next Post