Ni raha sana kwenye mahusiano yako ukimpata mtu ambae mnapendana kwa kila hali kwani wataalmu wa masuala ya saikolojia wanasema itakuongezea siku za kuishi na kukufanya uwe mwenye furaha siku zote.
Katika hali ya kawaida maisha yanabadilika kila kukicha hivyo kuna ugumu kidogo kumpata mtu ambae mtaendana nae na kuishi kwenye ndoa au hata kwenye uchumba mpaka kuja kuona nae hapo ndiyo kwenye msingi wa ndoa yenyewe kwani mkikurupuka furaha utaisikia tuu kwa wenzio.
Kwa miaka ya hivi karibuni ndoa zinaonekana kuvunjika sana sababu kubwa ikiwa ni mabadiliko ya kiuchumi,tamaa,ulemavu wa ukubwani,ugumba huku wengine wakienda mbali hata kusiingizia umri.
Katika imani ya baadhi ya dini hurusu mke/mme kuomba talaka ya kuachana huku imani nyingine wanaamini kuwa ndoa ni kiapo ambacho kamwe hakiwezi kutenganishwa na binadamu mpaka mmoja wenu afariki dunia ndiyo upate ruksa ya kutafuta mwingine.
Anyway ushawahi kujiuliza ghafla mtu uliyenae kwenye uchumba au ndoa akatangaza kuachana na wewe kwa sababu zake binafsi na wewe ndiyo ulimtegemea kwa kila kitu kwenye maisha yako? utafanya nini?
Bila shaka ni kipindi kigumu sana katika mahusiano kwani ni muda ambao kama hautapata ushauri basi huenda ukapatwa na msongo wa mawazo au hata kupoteza uhai wako kwani takwimu kutoka Shirika la afya duniani (WHO) zinaonesha watu laki 8 duniani kote hupoteza maisha kwa msongo wa mawazo wengi wao wakiwa ni kuanzia miaka 15-29 na kesi nyingi hutokana na mahusiano.
Kama umepatwa na matatizo hayo ya kuachwa au ndiyo penzi lako lipo njia panda basi ni muda wa kujiandaa kisaikolojia ili usijekupatwa na majanga kwani watu wengi baada ya kuachwa na wapenzi wao huishia pabaya kutokana na kutojiandaa.
Haya ni mambo 10 ambayo hutakiwi kuyafanya kama utataka kuishi kwa furaha baada ya kuachana na mpenzi wako au baada ya ndoa yako kuvunjika.
1.Epuka kulipiza kisasi, mwachie Mungu na kubali yote yaliyotokea na kuruhusu yapite.
Unapoachwa ni kama adhabu fulani hivi kwani akilini mwako utajiona kama huna thamani na kuanza kujitoa kasoro kwa kujiuliza maswali kibao mfano sikumridhisha, sina mvuto na mambo mengi utafikiria.
Kipindi hiki unashauriwa kufunga mlango kabisa kwa ex wako tena ikubali hali hiyo ikupite ili ukaribishe maisha mengine ya furaha huku ukimuomba Mungu kwa sana.
2.Epuka kusikiliza nyimbo za huzuni au kubembeleza
Baada ya kupigwa chini na mpenzi wako, epuka kusikiliza nyimbo za huzuni au mapenzi zenye kubembeleza hizi zitakufanya ufikirie majanga yaliyokukuta badala yake sikiliza nyimbo za kufurahisha zenye kuchezeka na zenye kukufanya ujione wewe ni mshindi muda wote na mwenye furaha.
3.Epuka kuita mahusiano yako ni magumu (Complicated).
Watu wengi hususani wanawake wanapoulizwa na wanaume kuhusu status zao za mahusiano asilimia kubwa majibu yao nina mtu lakini tumezinguana, majibu ambayo huwafanya waumie kisaikolojia hii ni kutokana na kujiona kuwa umri unaenda na bado hawajapata mtu wa kuishi nae.
Hiki kitu huwapata wanawake kwani huwa ni wagumu sana kuruhusu mioyo yao kusahau mapema vitu kutoka kwa ex wao nakumbuka mwaka 2014 Amber Rose alivyomwagana na WizKhalifa alikuwa akilalama kila siku mitandaoni akiamini hiyo itampunguzia machungu kumbe ndiyo kwanza ilimzidishia machungu.
Post a Comment