Ifahamike kuwa hakuna asiyehitaji mapenzi ya kweli ingawa kuna wapenzi wanaothamini penzi kwa
mwenzi wake anapokuwa na pesa au kazi Fulani na baada ya hapo hujitoa katika mahusiano hayo haliambayo huleta kwikwi katika mtima wa moyo wa anayefahamu kupenda.
1…MUONGO.
Hakuna asiyefahamu athari za mtu muongo katika jamii, vivyo hivyo ndivyo ilivyo katika mapenzi uongo
ni sumu mbaya na nidalili moja wapo ya kuonyesha kuwa mpenzi wako hana penzi la dhati nawe na
huyo aweza kukuletea athari za kufikiri hapo baadae endapo hautakuwa makini nae.
Hivi utajisikiaje Mpenzi wako akigundua kuwa ulikuwa
ukimdanganya na hatimaye yeye akajua ukweli wa suala ulilokuwa ukimpiga fiksi? Lakini ushauri wangu si kumuacha bali jaribu kumshauri kwa hekima na
akiendelea na tabia hiyo ujue kuwa hana mapenzi ya kweli kwako.
2..KUPENDA SANA PESA.
Ukiona mpenzi wako wa kike ama kiume anapenda sana kupata pesa kutoka kwako tambua ni moja ya
dalili ambazo zinajieleza kuwa hana mpango nawe bali analazimika kuwa nawe kutokana na pesa ama
kipato chako.
Mpenzi wa namna hiyo ili kujihakikishia dalili hii siku
moja akikuomba pesa hata kama ameziona mwambie kuwa huna,hapo yupo tayari kuvunja hata
mahusiano kwasababu kitu muhimu kwake hajapata na wala wewe si muhimu tena kwake.
Nieleweke kuwa sisemi pesa ni mbaya katika mapenzi, la hasha bali pesa na mapenzi ni sawa na trafiki na kondakta katika mambo Fulani yale………ya kuchafua mifuko kwenye nguo nyeupe……………na ni
muhimu wapenzi mkapenda kupeana maarifa ya kufanya kazi halali ili kujipatia vipato kwa ajili ya kuepukana na hili.
3…HAJALI KUTOKUA PAMOJA NA WEWE.
Mpenzi anaye kupenda muda mwingi hutamani kuwa nawe karibu na inapotokea hamjaonana hata
masaa sita au matatu hujisikia shida ambapo kwa wengine hufikia kupiga simu na ukimuuliza
anasemaje atakuuliza maswali yaliyoshonana kama ushanga mara upo wapi? Umekula? Na upo na
nani? Na maswali mengi ya namna hiyo ili mradi moyo wake utulie.
Endapo Mpenzi wako mkiwa mbali naye kwa muda wa masaa mengi na yeye akaonyesha kuwa hakukosa
chochote kutokuwa nawe karibu ama kuwasiliana nawe basi ujue kuwa mpenzi huyo ni kimeo yaani
hana mapenzi ya dhati kwako.
4…ANAPENDA KUKUUDHI.
Dalili ya Nne ya mpenzi asiyekuwa na mapenzi ya dhati nawe ni yule anayependa kukuudhi mara kwa
mara kana kwamba anatafuta sababu ya kuachana nawe lakini anashindwa kutamka bayana kuwa haitaji tena kuwa nawe.
Maudhi hayana budi kutokea pale inapobidi kwa bahati mbaya sana na si kwa makusudi, lakini wapo
wapenzi wanaowaudhi wenzao kwa makusudi huku wakiendelea kusisitiza maudhi hayo kama utani
na kujua kwa makusudi kuwa anamuumiza mwenzi wake bila kuomba msamaha.
Ingawa kuomba msamaha ni kipaji na hasa katika
mfumo dume ambao unaonesha kuwa mwanaume anapoomba msamaha basi ujue katumia njia
nyingi za kumaliza tatizo hilo zimeshindikana hivyo kaomba msamaha kwa kulazimika sana na
kwa siri.
Post a Comment