- Anakuwa Na Aibu Kali Anapokuwa Nawe. Hii dalili ni ya kimwili, na humtokea mwanamke anayekupenda kweli. Ghafla anakuwa na hofu unapokutana nae na unapokuwa nae karibu. Kujihakikishia hilo pia, jaribu kuongea nae uso kwa uso, ukiona shahuku na wasiwasi vinazidi, ujue kuna uwezekano mkubwa amekuzimia.
- Anaonyesha Tabia Za Kitoto Anapokuwa Nawe. Mara kadhaa, mwanamke anayekupenda kimapenzi huonyesha tabia za kitoto. Utamuona anaongea kwa sauti ya juu, anarukaruka, au anacheka kwa sauti, kukufanya umuangalie/umzingatie anachofanya. Na angalia pia anapo ongea, sauti yake ataifanya ya kitoto na kudeka hivi. Na hapo mara nyingi anategemea umuonyeshe kama unamjali. Muonyeshe kwamba unamjali na upo tayari kumlinda na kumjali vilivyo.
- Anakupa Zawadi Za Kipekee. Ingawa si zawadi zote ukipata kutoka kwa mwanamke, inamaanisha anakupenda kimapenzi, lakini, mwanamke akikupa zawadi, huashiria kwamba amekuthamini kwa kiasi kikubwa “You are someone special”. Kuwa makini kujua kama zawadi anayokupatia ni special, au ni zawadi tu yakawaida kama anayowapatia rafiki zake wengine. Angalia Anavyokupatia zawadi, kama atakupatia zawadi na kuonyesha kujali, kukiambatana na maneno au barua, kuna dalili kubwa anakuzimia huyo.
- Anauliza Maswali Mengi Juu Ya Maisha Yako. Kama mwanamke amevutiwa nawe, atauliza maswali mengi juu ya maisha yako. Maswali huwa madogo madogo, kama kutaka kujua vitu unavyo vipenda, na mengine hulenga kujua mipango yako ya baadae. Na mara nyingi huhitaji maelezo ya kina kama akiona majibu yako hayamtoshelezi. Ukigundua mwanamke amevutiwa nawe na ameanza kuuliza maswali mengi, jaribu kumpa maswali yatakayo mvutia. Lakini hakikisha humdanganyi, kuwa mkweli kwa kila unacho mueleza, kwani kunanganya kutaleta matatizo hapo baadae akigundua ukweli.
- Anajitahidi Kuanzisha Mazungumzo. Kwa kawaida mwanaume ndio huwa anaanzisha mazungumzo, kwa kuuliza maswali ya kichokozi na kuanzisha hoja ili kupata ushiriki wa mwanamke mlengwa katika mazungumzo. Ukiona mwanamke huyo anachangamkia sana maongezi kuliko kawaida, kuna uwezekano mkubwa amevutiwa nawe. Mwanamke anayekupenda kimapenzi hupendelea kutumia muda mwingi kuongea nawe. Na mara maongezi yanapoishia, hutafuta hoja mpya ya kujadili, ili tu muendeleze maongezi.
- Ataonyesha Kupenda Vitu/Hobbies Ambazo Unazipenda Pia. Utakuta ghafla, anaanza kusikiliza nyimbo unazozipenda pia, au kuuliza maswali mengi juu ya hobbies zako. Na ataanza kukuomba mshiriki pamoja kwenye michezo unayoipenda, au kuangalia vipindi vya TV pamoja, au kushiki katika shughuli Fulani ambayo unaifanya muda mwingi . Kunauwezekano mkubwa anahitaji kuwa karibu nawe ili kukujua vizuri. Hii inaweza ashiria mwanamke huyo anakupenda.
- Hujaribu Kukushawishi Kwa Kujiweka Katika Muonekano Utakaokuvutia. Angalia style za nywele, nguo, viatu, vipodozi, na anvyoonekana kwa ujumla. Kma utagundua anafanya jitihada yaw ewe kumuona mzuri, kunauwezekano anahitaji wewe uvutiwe naye. Ukigundua hilo, jaribu kumsifia juu ya vile anavoonekana na mfanye ajisikie jitihada alizoweka kujiandaa zimezaa matunda, na kuona kwamba unamjali sana.
- Anaonekana Ni Mwenye Furaha Muda Wote Anapokuwa Nawe. Mwanamke huonyesha uchangamfu pale anapokuwa karibu na mtu anae mpenda. Chunguza macho yake, tabasamu, na vitendo. Kama akionekana ni wenye furaha, kuna uwezekano anafurahia kuwa karibu nawe. Hakikisha unaonyesha kumjali na endapo anafarijika sana uwepo wako na vile unavyo mfanyia, kunauwezekano mkubwa tayari amekuzimia huyo.
- Hujaribu Kuku Angalia Kwa Kuibia Ibia Hivi. Kwa mara kadhaa, mwanamke anae kupenda, hujaribu kukuangalia sana kwa kuibia ibia, tena kwa aibu, ili usigundue anakuangalia. Na hukwepesha macho faster pale unapogeka kumuangalia. Mara nyingi utajikuta unamkamata anakuangalia. Jaribu pia kumuangalia usoni pale mnapo ongea, ukiona kunamabadiliko fulani kila unapomtazama usoni, jua kuna uwezekano amekuzimia, na kama unampenda kweli usipoteze muda mwambie unavyo jisikia kwake.
- Hujaribu Kuku Onyesha Kuwa Anakujali. Hujitolea vitu vingi kwa ajili yako, na hupenda kukuona muda wote unafuraha. Huwa na wasiwasi pale anapogundua una matatizo fulani, na hujitahidi kukuonyesha kuwa yupo nawe pamoja, pale unapo muhitaji.
- Hupenda Kuchat Muda Mrefu Na Wewe. Hujibu text zako zote, na mara nyingi haraka zaidi kabla ya wewe kumjibu. Mara nyingine hutuma messages na kudai ametuma kwa bahati mbaya. Ukiona hivyo ujue anahitaji kuchat na wewe, ila tu hataki kukuonyesha kwamba anajikomba sana kwako.
- Huonyesha Wivu, Haswa Pale Unapokuwa Karibu Na Wanawake Wengine. Mwanamke anaekupenda, akiona kuna wanawake wengine wanakupa compan, ataonyesha wivu wa hali ya juu. Na hii ni moja ya dalili za juu sana kumjua mwanamke kama anakupenda kimapenzi.
- Hukumbuka Kila Kitu Unacho Kiongea. Atasahau vitu vyote, lakini hukumbuka kila neno unaloongea. Na zaidi huwa mtu wa kwanza kukukumbusha kama kuna kitu umesahau. Zaidi zaidi hukumbuka tarehe yako ya kuzaliwa na huwa wa kwanza kuku takia happy birthday.
Post a Comment