SMS ZA KUOMBA MSAMAHAA KWA MPENZI NAKUOMBA KURUDIANA.








Hivi kweli haya ndiyo mapenzi ama naota
njozi? Nimefanya kila naloweza kuliimarisha
letu penzi lakini naishia kuambulia majonzi,
nimekuwa mtu wa kububujikwa na machozi
kwa sababu ya lako penzi, kama nimekukosea
tafadhali niwie radhi mpenzi, nakupenda na
amini wewe pekee ndiye uliyetimiza ndoto
yangu ya mapenzi.
______________________________________
Hivi ni kosa gani nilililokutendea ambalo
sipaswi kusamehewa? Ni kweli nilikosea
nahitaji kusamehewa mpenzi, plz naomba
nielewe kwani sina mwingine zaidi yako
wewe. Luv u
_______________________________________
Nakiri kweli nimekukosea naomba wako
msamaha kwa yote yaliyotokea hakika
nimekukwaza
lakini kwa hakika hii ni mara yangu ya kwanza
naamini,naamini utanisamehe laaziz
na kunipa nafasi ya kulienzi lako penzi.
_______________________________________
unajua nakupenda ila tu umeamua kunitenda
rudisha moyo nyuma kasha twende
sambamba mapenzi yanavyokwenda.
_______________________________________
Mapenzi ni usaníi ukiigiza utashindwa,mapenzi
yanatoka moyoni wengi walioigiza
walishatengana,mpenzi wangu usiniache.
______________________________________
penzi la kweli siku zote hudumu,penzi la
kitapeli haliishi ugomvi,mpenzi wangu leo
nimegundua nakukosea na naahidi kubadilika
na kuwa mpenzi mpya na bora,nisamehe . .
_______________________________________
mpenzi nashukuru nikikuacha nitakuwa
ninakufuru mi ndiyo mpenzio na hauna
mwenzako mpenzi kuwa huru.
_______________________________________
Japo umeniuzi sina budi kukupa hizi pongezi,
sijui umejifunza wapi mapenzi, hakika kwako
mi ni mfungwa wa mapenzi! Nakupenza
mpenzi nitunziye langu penzi!
_______________________________________
Hakika sikutaraji kulikosa lako penzi, wataka
kuniacha kuniacha ningali nakuhitaji, mpenzi
tambua nahitaji yako hifadhi na niko radhi
kukupeleka hadi kwa wangu wazazi, amini
kwenda kwa mwingine sihitaji. Nakupenda.
_______________________________________
Siamini kilichotokea, hakika nimekukosea,
lakini naapa katu sitorudia, upuuzi
niliokufanyia, najua jinsi gani waumia ndiyo
maana umeninunia, nisamehe mpenzi nafsi
yangu ipate kutulia kwani bila wewe sin
thamani katika hii dunia!
_______________________________________
Kina ninapokukumbuka machozi yanidondoka,
hivi leo mwana wa mwenzio ninaumbuka kwa
kuparamia mapenzi kwa pupa, ukweli nakupa,
hivi sasa najuta! Nisamehe mpenzi.
_______________________________________
Ni kweli nakiri ndani ya nafsi yangu kwamba
nilikukosea mpenzi wangu, naomba unisamehe
na unipe nafasi nyingine katika moyo wako
mpenzi wangu. Nakupenda sana, pokea busu Mwanana....mwaaaaaaaa.


Post a Comment

Previous Post Next Post