Niseme nini ujue nakupenda? Nifanye nini ujue nakupenda?
Nikuite jina gani ujue ni wewe peke yako upo moyoni
mwangu? Hakika hakuna ila moyo wangu ndio unaosema kuwa
nakupenda, niamini mpenzi
*°·.¸¸.° °·.¸¸.°*
upendo ni jibu kwamba kila mmoja anataka. . . .
upendo ni lugha ,
kwamba kila mmoja anaongea,
upendo hauwez kununuliwa,
na isiyo kadirika na ya bure,upendo kama uchawi safi,ni
siri ya maisha matamu
nakupenda mpenzi
*°·.¸¸.° °·.¸¸.°*
"Mimi sitaki kuwa kila kitu kwa kila mtu, lakini napenda
kuwa kitu kwa mtu.na mtu mwenyewe ni wewe"
nakupenda laazizi
"Kama mimi nilikuwa na maua kila wakati
mawazo yangu
yangekuwa juu yako,nisingefikiri wa kumpa mwingine kabla
yako je wewe ungekuwepo nayo
ungempa nani kwanza? "
*°·.¸¸.° °·.¸¸.°*
ningependa nikuambie neno ambalo halina gharama na
likutumiwa vibaya halina maana wala thamani. neno hilo
haliandikiki kwenye karatasi wala hata halitamkiki ila tu
Linatokea Bila kujua na halina sababu.neno hilo mi
mwenyewe silijui ila ndo linatufanya tuwe pamoja Japo tupo
Kasi Na Kusi. Nakupenda sana Dear
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
naukunjua moyo wangu huishi milele maishani ,nafungua
nafsi nikupende wewe pekee,nafunga milango ya moyo wangu
ili
kutokupokea ugeni wowote wa moyo zaidi yako
mpenzi.nakupenda sana laazizi
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
sipo tayari kuukabidhi moyo wangu kwa mwingine zaidi
yako,wewe ni wa pekee maishani mwangu mwenye kujua hisia
moyoni mwangu
mpenzi nipende daima pendo lako nitalienzi, nakupenda
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
mapenzi si pombe lkn yanalewesha, wala si kidonda lakini
yanatonesha,wala si maradhi lakini yanaumiza, wala si
njaa lakini yanakondesha ,mapenzi ni uvumilivu kwa
unaempenda
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
mapenzi ni safari=unifanye nauli ya moyo, mapenzi ni
maradhi=unifanye daktari ni kutibu maradhi yako,mapenzi ni
kiu=niwe maji jangwani,mapenzi ni chakula=nikulishe
maishani mwako na uwe asali moyoni mwangu
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
wengi hupenda fanta kwa ladha yake,wengine hupenda
pilipili kwa muwasho wake,wengine hupenda asali kwa utamu
wake ila mimi nakupenda wewe kwa upendo wako.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
nimetuma ndege wangu auzunguke ''moyo'' wako kwa '' upendo
'' auguse ''uso'' wako kwa ''faraja'' na mwisho
akunong'oneze sikioni taratibu kuwa nakupenda.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
mapenzi ni utoto,deka ulie nitakubembeleza,mapenzi ni
zawadi tabasamu nibusu niambie kiasi gani unanpenda,naweza
kusema asilimia kubwa jina lako limezunguka kuta wa moyo
wangu.kamwe jina lako haliwezi kufutika.nakupenda sana
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
teke la kuku halimuumzi mwanaye sawa na dhati ya mapenzi
haiumzi moyo wa ampendaye,tugombane sasa hivi tupatane
badaye,najua hakuna wasiogombana ,kama wapo siku
wakigombana wataachana.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
yapitayo mdomon yametokea moyon,uyaonayo hadharani
nimeagizwa na manani yakuridhishayo nafsini ni utamu wa
yakini.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
nakupenda sana mpenzi wangu ,we ndo wa pekee mwenye kujua
furaha ya moyo wangu nikiwa na majonzi huwa upo karibu
nami,nikiwa na furaha huja kushea nami,ahsante wangu
tabibu ,we ndo wangu wa manani.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
kila niamkapo mawazo yangu huwa kwako na upepo uvumapo
huhitaji uwepo wako na hasa nikukumbukapo kumbato
lako,nakupenda mpenzi
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
Furaha yangu ni kuwa nawe kwani u zaid ya mboni
yangu,najisifu kuwa nawe maishani mwangu naamini itatokea
kutokuwa mbali nawe mpz wangu,unisahaulishe machungu na
karaha za huu ulimwengu .nakupenda dia
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
>>--------->>> Mshale huu unamtafuta mtu muhimu sana ktk
maisha yangu na kama umekutana nao
usiukwepe uache
uchome Moyo wako gharama
za matibabu juu yangu.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
sioni zawadi ya kukupatia kwa mapenzi
unayonipatia,
moyoni nimekuridhia wewe pekee penzi langu daima
kukupatia nakupenda
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
hakika kama ni mume MUNGU kanipatia,kuwa nawe najiona
kama malkia ,nakupenda mpz na daima nitaenzi penzi
lako.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
Nina habari nzuri nataka kukuambia kuna mgeni leo kaja
kunitembelea,nguo nyekundu amevalia yaani!utamu wako kwa
sasa siwezi kukupatia
kwa maana mgeni kashakuharibia
nakupenda dear
Post a Comment