=========================

Asubuhi na mapema mtoto amenijia


Kanipa mapenzi mema nikawa namsifia


Mahaba yake mwanana sijui wapi katoa

@@@@@@@@@@@@@@@@

Penzi lake marumaru kanipa nikapokea


Wala sio waruwaru museme hakutulia


Ni mcheshi hana paru mrembo ana vutia

=========================

Huyu wangu kisamwande siwezi kumkimbia


Yeye ndie my wanje ninae mtegemea


Niacheni nimpende mengi kashanifanyia


Kwake sikai upande medali nitanyakua

@@@@@@@@@@
Post a Comment