Ingawa mwaka umekwisha, mawazo yangu katu sitobadilisha, amini ni wewe pekee unayenipagawisha, hakika kwa penzi lako kiu yangu katu haitakwisha!
2. Ingawa kwa sasa u-mbali nami, sitaacha kukupenda, kumbuka ni mimi mwenyewe niliyekupenda, siioni sababu yakukutenda, amini ni wewe tu nayekupenda!
3. Raha ya upele upate mkunaji, utamu wa mtori upate anayejua kupekecha, raha ya penzi mpe anayejua kupenda! Mwenyewe nimekupenda unayejua kupenda, nakupenda ma luv.
4. Mpenzi najua mengi umeambiwa, shuruti roho inakuenda mbio, tafadhali punguza wasi niamini mwana wa mwenzio, usiye waamini, ukanimwaga mwenzio sina kimbilio.
5. Watu hufanya ubahili katika pesa, si katika mapenzi la azizi, sielewi kwa nini umeadimika siku hizi, si sms, simu jamani hata beep sizipati siku hizi! Nakupenda sijui kwa nini umedadilika siku hizi.
6. Laiti moyo ungekuwa na kifuniko basi ningekuwa radhi kukwambia fungua uone unavyokereketa, lakini sivyo, nimebaki nauguza vidonda, nieleze ninene nini ujue nakupenda kijana mwenzio…
7. Hakika moyo ukipenda inakuwa vigumu kuuzuia, kila nikuonapo rohoni naumia, mapigo ya moyo yanienda mbio, hutamani tuwe ulingoni, ujuzi tuoneshane pasipo na soni! Nakupenda mpenzi
8. Jua jembamba limechomoza, moyoni nakuwaza, ndotoni umenigalagaza, hakika wewe ndio wangu mwangaza, usiku kucha nimekuwaza, je, u hali gani?
9. Kiza kimeingia, hofu inaniingia, usingizi waninyatia, kulala nahofia, ulipo wataniibia, mpenzi tambua nakupenda toka moyoni, lala unono, hakikisha tunakutana ndotoni! Usiku mwema luv u.
10. Najua vile ulivyo bize kutafuka maisha, majukumu kuyakamilisha, tazama ukutani mchana umefika, umbali nami siwezi pika, tafadhali jongea mgahawani upate japo kitu fulani, lunch njema ma luv.
11. Jipe moyo mpenzi hakika utashinda, wahenga walinena ndoa ni ndoa, amini upo vitani, ukidumisha upendo, furaha na amani, ndoa yako itatoka mashakani! Pole kwa yaliyokufika!
12. Mtu gani usiye ridhika nimekupa hadi sisivyo simulika, lakini huishi kuhangaika, kutwa kugaagaa na upwa, kumbuka mgagaa na upwa hali…., hakika Mungu atakupa unachokitafuta, wewe hangaika.

Post a Comment