JINSI KUZUIA MIMBA KUTUNGA BAADA YA KUFANYA NGONO BILA KINGA.{EMERGENCY CONTRACEPTIVES PILLS]







Karibuni tena ndugu wasomaji wa SIRI ZA AFYA BORA, Kama tulivyosema mara ya mwisho kwamba tutakua tukiongelea makala za uzazi wa mpango kwa mda flani ili kuweka swala hili sawa kwa watu ambao hawafahamu.
Leo tutakua tukiongelea jinsi ya kuzuia ujauzito kama njia ya uzazi wa mpango kwa mwanamke aliyetembea na mwanaume na kua na wasiwasi amebeba mimba baada ya tendo hilo.
 Mwanamke huyu ni yupi?
  • ·        Ambaye hakutumia kinga wakati wa tendo la ndoa.
  • ·        Ambaye amebakwa au kulazimishwa kingono
  • ·        Ambaye kondomu imepasuka wakati wa tendo la ndoa.
  • ·        Ambaye ametumia vibaya njia yake ya uzazi wa mpango kama sindano au vidonge.
  • ·        Kama mwanaume alishindwa kuchomoa wakati wa kutoa mbegu.
Jinsi ya kutumia dawa baada ya matukio hayo.
dawa hizo zinatakiwa zitumike ndani ya siku tatu baada ya makosa hayo hapo juu kufanyika.
Dawa hii hufanya kazi ya kuchelewesha yai kushuka kwenye mfuko wa uzazi ili mbegu za kiume zikutwe zimeshakufa.
Dawa hizo ni zipi?
dawa  nzuri kuliko zote inaitwa p2, inapatikana maduka ya madawa.meza kidonge kimoja kisha meza kingine baada ya masaa 12 na utakua salama.
Madhara madogo madogo ya dawa hizo…
  • ·        Kichefuchefu
  • ·        Tumbo kuuma
  • ·        Kuchoka sana
  • ·        Kichwa kuuma
  • ·        Kizunguzungu
  • ·        Kutapika
  • ·        Maumivu ya matiti.

Post a Comment

Previous Post Next Post