SIKU ISIISHE KAMA HUJAMTUMIA MPENZI WAKO SMS HIZI

 Mapenzi ni nini? Wale wasiopenda huita majukumu, wale wanaoyachezea huita mchezo, wale wasiokuwa nayo huita ndoto, na wale wanaoelewa huyaita mwisho wa safari, na mimi, mwisho wangu ni wewe.
 Ni mapenzi gani yanayofanya simu yako ilie kila nitumapo meseji?
 Kama mapenzi huweza kukimbiwa kwa kufumba macho yetu tu, basi nisingefunika macho kabisa. Sitaki sekunde ipite bila kukupenda wewe.
 Nilikuwa nikifiria kwamba ndoto haziwezi kuwa kweli, lakini nilibadili mawazo yangu pale tu nilipokuona wewe.
 Baadhi ya watu huzaliwa na vipaji. Huweza kufanya mambo mazuri kwa ujuzi wao, lakini hamna anayekufikia wewe, kwani ukinisogelea tu kila kitu huwa kizuri.
Mwanamke ni yule amfanyaye mwanamme auhisi uanaume wake, wewe ni mwanamke mwenye sifa hizo.

Post a Comment

Previous Post Next Post