HUBA NI WEWE TU MPENZI WANGU


Sijawahi kupata mapenzi ya kushiba kama unipayo wewe mpenzi wangu

Ni mimi nilokupenda,Ni mimi nilokuchagua na ni mimi nitakayekuoa Nakupenda my sweet wangu

Ya walimwengu usiyape nafasi Waache wapambane na hali zao

chuki fitina zinawatoa kamasi Waroge matunguri bado sitokuasi me kiboko yao

Babe Nachojua Nakupenda sana

Moyo wangu umekuchagua nakuwaza usiku mchana

Ukiniacha nitazidi pungua kwa mawazo nitakondeana

Mtoto mapenzi unayajua sio siri umesomea una PhD 

Najuta kwa nini mapema sikukujua  mpka wahuni ujanja wakanizidi

Maumivu makali makali nikaugulia mpka nikakutana nawe langu waridi

Kukupata wewe najisifia waache wajue nafaidi
Tafadhali usinitende wangu malkia Nakupenda sana My lovely you

Post a Comment

Previous Post Next Post