UTAMU NA UBAYA YA WANAWAKE WANENE.

"Lazima ujue kutofautisha kati ya msalaba na jumlisha kuna x na kuzidisha”. Si maneno yangu hayo ni maneno yake Diamond Platnumz kwenye wimbo wake wa NITAMPATA WAPI vivyo hivyo katika sifa za binadamu zipo hivyo tumetofautiana kitabia kulingana na maumbile yetu.

Leo katika Kona ya Mahaba tumekuandalia faida za Mwanamke Mnene katika mapenzi ili upate kutambua thamani ya kila mmoja na utambue kila kitu kipo kwa makusudi na si kwa bahati mbaya; 



Hivyo utamu wa mwanamke mnene hutokana na vitu vifuatavyo karibu twende sawa uzitambue kwa usahihi sifa na tabia za mwanamke mnene.

Wepesi wa kusamehe

Mwanamke mnene mara nyingi huwa ni mwepesi wa kusamehe pale anapokwazwa na mtu; hapendi kuweka vinyongo moyoni.

Wanapenda kuomba radhi

Wataalamu wa mahusiano wanasema wanawake wenye maumbo makubwa wanasifa ya kuomba radhi pale wanapokosea.

Wanatulia kwa mwanaume mmoja

Takwimu zinaonesha wanawake wanene sio viruka njia; mara nyingi hutulia katika mahusiano na kudumu na mwanaume mmoja kwa kipindi kirefu.

Wakipenda wanapenda kweli

Wanawake wanene wanatabia ya kupenda kwa dhati mara wanapoingia katika mahusiano; watu hawa husifika kwa kuwa na mapenzi ya dhati kwa wapenzi wao.

Sio wabishi

Wanawake wanene hawana silka ya ubishi, inasemekana wanawake wembamba ndio wenye tabia ya ubishi lakini kwa upande wa wanawake wanene hawana tabia ya mabishano na hawapendi kujiingiza katika ubishi.

Wanajua kudeka na kudekeza

Wataalamu wa mahusiano wanasema kwa asili wanawake wenye miili mikubwa wanapenda kudeka na kudekezwa katika mapenzi; kwa kufanya hivyo hujikuta wakidumu kwa kipindi kirefu katika mahusiano yao.


Watiifu

Kwa asili yao wanawake wanene ni wanyenyekevu na watiifu kitu ambacho si rahisi kukuta kwa kila mwanamke. Bila shaka utii wao ndio unaowasaidia katika kudumisha mahusiano yao.

Hawaringi sana

Inasemekana wanawake wenye maumbile makubwa hawana tabia ya kujivuna wala kujikweza wanauwezo wa kuishi na watu wa aina yoyote kwa sababu ya unyenyekevu walionao.

Wanasahau haraka

Moja ya hasara walionayo wanawake wanene ni tabia ya kusahau mambo kwa haraka. yawezekana hali hii huwapata kutokana na kuwa na uwezo mdogo wa kutuna kumbukumbu.

Vizazi vyao vinaakili timamu.

Utafiti uliofanywa hivi karibuni na wataalamu wa afya umebaini wanawake wenye maumbo makubwa huzaa watoto wenye akili nyingi.

Post a Comment

Previous Post Next Post